Kusambaza Mipangilio ya Kupokea Faksi kwa Masharti Yaliyobainishwa

Unaweza kuweka mipangilio ya usambazaji ili kupokea faksi kutoka kwa mtumaji aliyebainishwa au muda uliobainishwa.

Wakati hali nyingi (Masharti ya Hifadhi/Sambaza) zimewekwa, zimerejelewa katika mpangilio wa vipengee, na Masharti ya Hifadhi/Sambaza inayolingana kwanza inatekelezwa.

Unaweza kuweka mipangilio ya usambazaji hadi eneo, anwani ya barua pepe, folda ya pamoja, akaunti ya wingu au mashine nyingine ya faksi kutoka kwa mtumaji aliyebainishwa au muda uliobainishwa.

Kumbuka:
  • Iwapo unataka kufanya mipangilio ya kusambaza faksi zilizopokewa, kwanza ongeza anwani inayosambazwa kwenye orodha ya anwani au orodha ya anwani ya wingu. Tazama jedwali linalofuata ili kupata orodha ya kusajili.

    Aina ya Ufikio

    Waasiliani

    Wingu Orodha ya Mafikio

    anwani ya barua pepe

    folda ya pamoja

    akaunti ya wingu

    mashine nyingine ya faksi

Kuweka Mipangilio ya Usambazaji ili Kupokea Faksi kwa Masharti Yaliyobainishwa

Kumbuka:
  • Kando na kutumia paneli dhibiti ya kichapishi, unaweza kutumia Web Config kuweka mipangilio ya usambazaji ili kupokea faksi. Teua kichupo cha Fax > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Masharti ya Hifadhi/Sambaza, teua nambari ya kisanduku cha siri na kisha uteue Edit na uweke mipangilio ya eneo la kusambazia.

  • Unaweza kuchapisha na/au kuhifadhi faksi zilizopokelewa kwa wakati mmoja. Weka mipangilio kwenye skrini ya Edit iliyotajwa hapa juu.

  1. Teua Mipangilio kwenye paneli dhibiti yakichapishi, kisha uteue Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi.

  2. Teua Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Masharti ya Hifadhi/Sambaza, kisha gusa kisanduku ambacho hakijasajiliwa chini ya Masharti ya Hifadhi/Sambaza.

    Kumbuka:

    Iwapo unataka kubadilisha mipangilio ya kikasha kilichosajiliwa, donoa na ubadilishe mipangilio.

  3. Teua kikasha cha Jina na uingize jina unalotaka kusajili.

  4. Teua kikasha cha Hali ili kuunda mpangilio wa masharti.

    • Ulinganisho wa Kitambulisho cha Faksi cha Mtumaji: iwapo nambari ya faksi inayoingia inalingana na masharti uliyoteua kwenye kipengee hiki, kichapishi huhifadhi na kusambaza faksi zilizopokewa.
      Teua mashart ya Ulinganisho wa Kitambulisho cha Faksi cha Mtumaji na uingize nambari ya faksi (idadi ya juu ya dijiti 20) kwa kuteua kikasha cha KITAMBULISHO.
    • Uli'shaji kamili anwani ndogo (NDOGO): iwapo anwani ndogo (SUB) inawiana vilivyo, kichapishi huhifadhi na kusambaza faksi zilizopokewa.
      Wezesha mpangilio wa Uli'shaji kamili anwani ndogo (NDOGO) na uingize nenosiri kwa kuteua kikasha cha Anwani ndogo(NDOGO).
    • Ulinganishaji kamili wa nywila: iwapo nenosiri (SID) limewianishwa vilivyo, kichapishi huhifadhi na kusambaza faksi zilizopokewa.
      Wezesha mpangilio wa Ulinganishaji kamili wa nywila na uingize nenosiri kwa kuteua kikasha cha Nywila(SID).
    • Wakati wa Kupokea: kichapishi huhifadhi na kusambaza faksi zilizopokewa wakati wa kipindi maalum cha muda.
      Wezesha mpangilio wa Wakati wa Kupokea na kisha uweke muda katika Muda wa Kuanza na Muda wa Mwisho.
  5. Teua Hifadhi/Sambaza Mfikio, na kisha uweke mipangilio ya eneo la kusambazia.

    Teua Sambaza.

    Donoa Sambaza ili kuweka hii kwa On.

    Teua Mfikio > Ongeza Ingizo, kisha uteue maeneo ya kusambazia kutoka kwenye orodha yako ya waasiliani au orodha ya ufikio wa wingu. Unaweza kubainisha anwani ya usambazaji.

    Kubadili orodha, donoa na kuteua (Wingu Orodha ya Mafikio), au donoa na kuteua (Waasiliani).

    Ukimaliza kuchagua anwani za usambazaji, gusa Funga.

    Hakikisha kwamba anwani ya usambazaji uliyochagua ni sahihi, na kisha uchague Funga.

    Katika Chaguo Wakati Us'zaji Um'dikana, chagua kama unataka kuchapisha hati zilizopokewa au kuzihifadhi katika Kisanduku pokezi ya kichapishi wakati usambazaji unakosa kufaulu.

    Donoa Sawa.

    Muhimu:

    Wakati Kisanduku pokezi au kisanduku cha siri kimejaa, upokeaji wa faksi unalemazwa. Unastahili kufuta hati kwenye kisanduku pokezi punde tu zinapoangaliwa. Idadi ya nyaraka ambazo zilishindwa kusambaza imeonyeshwa kwenye katika skrini ya nyumbani, kwa kuongezea kwenye kazi zingine zisizochakatwa.

    Kumbuka:

    Ili kuchapisha faksi zilizopokelewa kwa wakati mmoja, donoa Chapisha ili uweke hii iwe On.

  6. Teua Sawa ili ukamilishe Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza Mfikio.

    Kumbuka:

    Unaweza kuweka kichapishi kitume barua pepe kwa watu unaotaka kuwaarifu kuhusu matokeo ya usambazaji wa faksi wakati mchakato wa usambazaji ukikamilika. Ilivyo muhimu, teua Taarifa za Barua pepe, weka michakato na kisha uteue eneo unapotaka kutuma arifa kutoka kwenye orodha ya waasiliani.

  7. Teua Sawa hadi urejee kwenye skrini ya Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza ili kukamilisha Masharti ya Hifadhi/Sambaza.

  8. Teua kisanduku kilichosajiliwa ambacho ulifanya mpangilio wa masharti, na kisha uteue Wezesha.

Kumbuka:
  • Hii hukamilisha uwekaji mipangilio ya usambazaji wa masharti ya kupokea faksi. Unaweza kuweka Mipangilio ya Kawaida ilivyo muhimu. Kwa maelezo, angalia ufafanuzi wa Mipangilio ya Kawaida katika menyu ya Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza.

  • Ikiwa umechagua kabrasha la kushiriki kwenye mtandao, anwani ya barua pepe, au akaunti ya wingu kama mafikio wa usambazaji, tunapendekeza kwamba ujaribu kama unaweza kutuma picha hadi kwa ufikio.

    Teua Changanua > Barua pepe, Changanua > Folda/FTP ya Mtandao kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, teua mafikio, na kisha anzisha utambazaji.

    Ikiwa umeteua akaunti ya wingu, unaweza kufanya jaribio kwa kutuma picha ambayo imehifadhiwa katika kisanduku cha faksi kwenye ufikio huo. Teua Kasha la Faksi kutoka kwenye kidirisha cha kudhibiti kichapishi. Teua (Menyu ya Uhakiki) > Tuma mbele (Wingu) kwa kisanduku cha faksi ambapo picha yoyote iliyotambazwa imehifadhiwa kwayo, teua ufikio, na kisha uanze kutuma.