Teua njia ya muundo wa faili za JPEG. 1-juu ni ya kuchapisha faili kwa kila ukurasa. 20-juu ni ya kuchapisha faili 20 kwa kila ukurasa. Kiolezo ni ya kuunda uchapishaji wa kiolezzo kwa maelezo.
Tosheza Fremu
Teua On ili kupuna picha ili kuteshea kwenye muundo wa chapisho ulioteuliwa kiotomatiki. Ikiwa mgao uwiano wa data ya picha na ukubwa wa karatasi ni tofauti, picha hupanuliwa au kupunguzwa kiotomatiki ili pande zile fupi zilingane na pande fupi za karatasi. Upande mrefu wa picha hukatwa ikiwa unazidi upande mrefu wa karatasi. Kipengele hiki huenda kisifanye kazi kwa picha za panorama.
Ubora
Teua Bora kwa ubora wa juu wa uchapishaji, lakini kasi ya uchapishaji inaweza kupungua.
Tarehe
Teua umbizo la tarehe ambayo picha ilipigwa au kuhifadhiwa. Tarehe haichapishwi kwa baadhi ya miundo.