Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Mipangilio > Mipangilio ya Printa
Mipangilio ya Printa
M'gilio Chanzo Karatasi
Usanidi wa Karatasi
Chagua ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi uliyoingiza katika chanzo cha karatasi. Unaweza kufanya Mip. ya Kar'si U'ipenda kwenye ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi. Teua ili kurudi kwenye mipangilio ya mwisho uliyofanya.
Onyesho Otom. Usanidi wa Karatasi
Teua On ili kuonyesha skrini ya Usanidi wa Karatasi unapopakia chanzo cha karatasi. Ukilemaza kipengele hiki, huwezi kuchapisha kutoka kwenye iPhone, iPad au iPod touch ukitumia AirPrint.
Hali Tulivu
Teua On ili kupunguza kelele wakati wa kuchapisha, hata hivyo, hii inaweza kupunguza kasi ya uchapishaji. Kulingana na aina ya karatasi na mipangilio ya ubora wa kuchapisha uliyoteua, huenda kusiwe na tofauti katika kiwango cha kelele ya kichapishi.
Muda wa Kukausha Wino
Teua muda wa kukausha wino unaotaka kutumia unapotekeleza uchapishaji wa pande 2.Kichapishi huchapisha upande mwingine baada ya kuchapisha upande mmoja.Iwapo chapisho lako limepakwa wino, ongeza mpangilio wa muda.
Muungan. Kompyuta kupitia USB
Teua Wezesha ili kuruhusu kompyuta kufikia kichapishi inapounganishwa kwenye USB. Wakati Lemaza imeteuliwa, uchapishaji na utambazaji ambao haujatumwa kupitia muunganisho wa mtandao unazuiwa.
Ondoa Mipangilio Yote
Huweka upya Mipangilio ya Printa kwa chaguo-msingi yake.