Unaweza kuchapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao ili kuangalia hali kati ya kichapishi na kipanga njia pasiwaya.
Pakia karatasi.
Teua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani.
Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya
, na kisha ubonyeze kitufe cha OK.
Teua Mipangilio ya Mtandao > Ukaguzi wa Muunganisho.
Ukaguzi wa muunganisho unaanza.
Fuata maagizo kwenye skrini ya kichapishi ili kuchapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao.
Iwapo kosa limetokea, angalia ripoti ya muunganisho, na kisha ufuate suluhisho zilizochapishwa.