Chunga mkono au vidole vyako visikwame wakati unafungua au kufunga kitengo cha kitambazaji. La sivyo unaweza kujeruhiwa.
Usiwahi kugusa vitufe vilivyo kwenye paneli dhibiti wakati mkono wako uko ndani ya kichapishi. Ikiwa kichapishi kitaanza kufanya kazi, inaweza kusababisha majeraha. Kuwa makini usiguse sehemu zinazojitokeza ili uzuie majeraha.
Ondoa jalada la nyuma.

Ondoa karatasi iliyokwama kwenye jalada la nyumba.

Ondoa karatasi iliyokwama.

Ingiza jalada la nyuma katika printa.
Funga jalada la waraka iwako liko wazi.
Fungua kitengo cha kitambazaji kwa mikono miwili hadi kijifunge.
Ondoa karatasi iliyokwama.
Usiguse kebo tambarare nyeupe na sehemu angavu iliyo ndani ya kichapishi. Ukifanya hivyo unaweza kusababisha hitalifu.

Funga kitengo cha kitambazaji.

Kitengo cha kitambazaji kimeundwa ili kufunga taratibu na kukataa kidogo kama kuzuia vidole vyako kukamatwa. Endelea kufunga hata ikiwa unahisi inakataa kidogo.