> Kupakia Karatasi na CD/DVD > Kuweka Karatasi > Mipangilio ya Ukubwa na Aina ya Karatasi

Mipangilio ya Ukubwa na Aina ya Karatasi

Iwapo utasajili ukubwa na aina ya karatasi kwenye skrini inayoonyeshwa unapoingiza kaseti ya karatasi, kichapishi kinakujulisha ikiwa maelezo yaliyosajiliwa na mipangilio ya chapisho ni tofauti. Hii hukuzuia kupoteza karatasi na wino kwa kuhakikisha kwamba huchapishi kwenye ukubwa usiofaa wa karatasi au kuchapisha kwa rangi isiyofaa kutoka na kutumia mipangilio ambayo hailingani na aina ya katarasi.

Iwapo ukubwa na aina ya karatasi inayoonyeshwa ni tofauti na karatasi iliyopakiwa, teua kipengee ambacho unataka kubadilisha. Iwapo mipangilio inalingana na karatasi iliyopakiwa, funga skrini.

Kumbuka:

Unaweza kuweka mipangilio kwa urahisi kwa kusajili mkusanyiko unaotumika mara kwa mara wa ukubwa na aina ya karatasi kuwa unaopenda. Unaweza kuunda mipangilio ya karatasi kwa kuteua kuweka awali kulikosajiliwa. Ili kusajili mpangilio wa awali, teua Favorite Paper Settings, teua > katika skrini inayofuata kisha ubainishe ukubwa na aina ya karatasi.