Fungua kifuniko cha nafasi ya nyuma ya karatasi.

Telezesha nje miongozo ya kingo.

Pakia bahsha kwenye alama ya kati ya kishale ya nafasi ya nyuma ya karatasi huku sehemu inayoweza kuchapishwa ikielekea juu.
Pakia bahasha huku pigo lake likielekea upande wa kushoto.

Telezesha miongozo ya kingo kwenye kingo ya bahasha.

Trei towe inarefuka kiotomatiki unapoanza kuchapisha. Pia unaweza kuitelezesha nje kikuli mapema.