Kuna mbinu mbili zinazopatikana za kulemaza muuganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi); unaweza kulemaza miunganisho yote kwa kutumia paneli dhibiti ya kichapishi, au kulemaza kila muunganisho kutoka kwenye kompyuta au kifaa maizi. Sehemu hii hufafanua jinsi ya kulemaza miunganisho yote.
Wakati muunganisho wa Wi-Fi Direct wa (AP Rahisi) unalemazwa, kompyuta zote na vifaa maizi vilivyounganishwa kwenye kichapishi katika muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) vinatenganishwa.
Iwapo unataka kukata muunganisho wa kifaa maalum, kata muunganisho kutoka kwenye kifaa badala ya kichapishi. Tumia mojawapo ya mbinu zifuatazo ili kukata muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) kutoka kwenye kifaa.
Kata muunganisho wa Wi-Fi kwenye jina la mtandao la kichapishi (SSID).
Unganisha kwenye jina jingine la mtandao (SSID).
Donoa
kwenye skrini ya nyumbani.
Donoa Wi-Fi Direct.
Maelezo ya Wi-Fi Direct (AP Rahisi) yanaonyeshwa.
Donoa Start Setup.
Donoa Change Settings.
Donoa Disable Wi-Fi Direct.
Angalia ujumbe, kisha udonoe Disable the settings.
Wakati ujumbe wa ukamilisho umeonyeshwa, donoa Close.
Skrini hufunga kiotomatiki baada ya kipindi maalum cha muda iwapo hutadonoa Close.
Donoa Close.