Kuunda Mipangilio ya Wi-Fi kwa Usanidi wa Kitufe cha Kusukuma (WPS)

Unaweza kusanidi mtandao wa Wi-Fi kwa kubonyeza kitufe kwenye kipanga njia pasiwaya. Ikiwa masharti yafuatayo yatatimizwa, unaweza kusanidi kwa kutumia mbinu hii.

  • Kipanga njia pasiwaya kinatangamana na WPS (Usanidi wa Wi-Fi Uliolindwa).

  • Muunganisho wa sasa wa Wi-Fi ulitambuliwa kwa kubonyeza kitufe kwenye kipanga njia pasiwaya.

  1. Donoa kwenye skrini ya nyumbani.

  2. Donoa Wi-Fi (Recommended).

  3. Donoa Start Setup.

    Iwapo tayari muunganisho wa mtandao umesanidiwa, maelezo ya muunganisho yanaonyeshwa. Donoa Change Settings ili kubadilisha mipangilio.

  4. Donoa Push Button Setup (WPS).

  5. Shikilia chini kitufe cha [WPS] kwenye kipanga njia pasiwaya hadi taa ya usalama imweke.

    Ikiwa hujui kilipo kitufe cha [WPS], au hakuna vitufe kwenye kipanga njia pasiwaya, tazama hati iliyotolewa yenye kipamnga njia pasiwaya kwa maelezo.

  6. Donoa Start Setup.

  7. Donoa Close.

    Skrini hufunga kiotomatiki baada ya kipindi maalum cha muda iwapo hutadonoa Close.

    Kumbuka:

    Iwapo muunganisho utashindikana, washa upya kipanmga njia pasiwaya, kisogeze karibu na kichapishi, na ujaribu tena. Iwapo haitafanya kazi, chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao na uangalie suluhisho.

  8. Donoa Close kwenye skrini ya mipangilio ya muunganisho wa mtandao.