> Kupakia Karatasi na CD/DVD > Kuweka Karatasi > Matini kuhusu Kupakia Karatasi

Matini kuhusu Kupakia Karatasi

Kichapishi hiki kina vyanzo vitatu vya karatasi. Pakia karatasi la ukubwa na aina inayofaa ili kukidhi mahitaji yako ya uchapishaji.

Nafasi ya nyuma ya karatasi

  • Unaweza kupakia laha moja la aina zote au karatasi inayoauniwa.

  • Pia unaweza kupakia karatasi nene (hadi unene wa 0.6 mm), karatasi ya ukubwa mdogo kama vile kadi za biashara, na karatasi iliyowekwa pamoja awali, ambayo haiwezi kupakiwa kwenye mkanda wa karatasi.

Mkanda 1 wa karatasi

  • Unaweza kupakia laha anuwai za karatasi ya picha ya ukubwa mdogo.

  • Iwapo utapakia karatasi sawa kwenye mkanda 1 wa karatasi na mkanda 2 wa karatasi na uteue Cassette 1→2 kama chanzo cha karatasi, kichapishi kinaingiza karatasi kiotomatiki kutoka kwa mkanda 2 wa karatasi wakati karatasi zinaisha kwenye mkanda 1 wa karatasi.

Mkanda 2 wa karatasi

Tunapendekeza kupakia karatasi tupu ya ukubwa wa A4 kwa kuwa hii inatumiwa mara kwa mara.