Kubadilisha kutoka muunganisho wa USB hadi Mtandao

Kutumia kisakinishaji na uwekaji upya katika mbinu tofauti ya muunganisho.

  • Kusanidi kutoka kwenye tovuti

    Fikia tovuti ifuatayo, kisha uingize jina la bidhaa. Nenda kwenye Mpangilio, na kisha uanze kusanidi.

    http://epson.sn

  • Sanidi kwa kutumia diski ya programu (kwenye modeli zinazokuja na diski ya programu na watumiaji walio na kompyuta za Windows zilizo na viendeshi vya diski pekee).

    Chomeka diski ya programu kwenye kompyuta, kisha ufuate maagizo ya kwenye skrini.

Uteuaji wa Kubadilisha Mbinu za Muunganisho

Fuata maagizo ya kwenye skrini hadi skrini ya ifuatayo ionyeshwe.

Teua Badilisha mbinu ya muunganisho ya printa (kwa kipangishi njia kipya cha mtandao au kubadilisha USB kwa mtandao, nk.) kwenye skrini ya Teua Shughuli Yako, na kisha ubofye Ifuatayo.

Chagua Unganisha kupitia mtandao pasi waya (Wi-Fi), na kisha ubofye Ifuatayo.

Fuata maagizo ya kwenye skrini.