Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Mipangilio > Mipangilio ya Printa
Mipangilio ya Printa
M'gilio Chanzo Karatasi
Usanidi wa Karatasi
Chagua ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi uliyopakia kwenye chanzo cha karatasi.Unaweza kufanya Mip. ya Kar'si U'ipenda kwenye ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi.
Usanidi wa Karatasi
Teua On ili kuonyesha skrini ya mipangilio ya karatasi kiotomatiki kwa kurejelea Mipangilio > Mipangilio ya Printa > M'gilio Chanzo Karatasi > Usanidi wa Karatasi wakati karatasi imepakiwa kwenye chanzo cha karatasi. Ukilemaza kipengele hiki, huwezi kuchapisha kutoka kwenye iPhone, iPad au iPod touch kwa kutumia AirPrint.
CD/DVD
Hurekebisha uelekeo wa uchapishaji wa CD/DVD kwa kusogeza juu, chini, kushoto, au kulia ili kutosheleza.
CD Ya ndani/Nje
Hurekebisha mwelekeo wa kuchapisha wa vipenyo vyaa ndani na nje vya CD/DVD. Hadi 120 mm ya kipenyo cha nje, na kiwango cha chini cha 18 mm cha kipenyo cha ndani kinaweza kubainishwa. Kulingana na mpangilio wa eneo la kichapishi, CD/DVD au trei ya CD/DVD huenda vikachafuka. Weka masafa ili kutosheleza aneo linalochapishika ya CD/DVD yako. Eneo la kuchapisha lililowekwa hapa ni thamani ya kwanza unapochapisha picha kutoka kwenye kadi ya kumbukumbu kwenye CD/DVD.
Vibandiko
Hurekebisha uelekeo wa uchapishaji wa kibandiko cha picha kwa kusogeza juu, chini, kushoto au kulia ili kutosheleza.
Karatasi Nyembamba
Teua Washa ili kuzuia wino kumwagika kwenye machapisho yako, hata hivyo, hii inaweza kupunguza kasi ya uchapishaji.
Hali Tulivu
Teua On ili kupunguza kelele wakati wa kuchapisha, hata hivyo, hii inaweza kupunguza kasi ya uchapishaji. Kulingana na aina ya karatasi na mipangilio ya ubora wa kuchapisha uliyoteua, huenda kusiwe na tofauti katika kiwango cha kelele ya kichapishi.
Muda wa Kukausha Wino
Teua muda wa kukausha wino unaotaka kutumia unapotekeleza uchapishaji wa pande 2.Kichapishi huchapisha upande mwingine baada ya kuchapisha upande mmoja.Iwapo chapisho lako limepakwa wino, ongeza mpangilio wa muda.
Mwelekeo
Teua Washa ili kubadilisha uelekeo wa chapisho; Huchapisha wakati kichwa cha chapisho kinasonga upande wa kushoto na kulia.Ikiwa mistari mlalo na wima kwenye nakala yako inaonekana kuwa ina ukungu au haijalinganishwa, kulemaza kipengele hiki kunaweza kutatiza tatizo hilo; hata hivyo, kufanya hivyo kunaweza kupunguza kasi ya chapa.
Ondoa Mipangilio Yote
Huweka upya Mipangilio ya Printa kwa chaguo-msingi yake.