Bainisha masafa ya chapisho. Hadi 120 mm ya kipenyo cha nje, na kiwango cha chini cha 18 mm cha kipenyo cha ndani kinaweza kubainishwa. Kulingana na mpangilio wa eneo la kichapishi, CD/DVD au trei ya CD/DVD huenda vikachafuka. Weka masafa ili kutosheleza aneo linalochapishika ya CD/DVD yako.
chapisha kwenye CD/DVD, Jaribu kuchapisha kwenye karatasi ya A4
Teua iwapo utachapisha CD/DVD ili kuunda chapisho la jaribio kwenye karatasi tupu ya ukubwa wa A4. Unapoteua Jaribu kuchapisha kwenye karatasi ya A4 unaweza kuangalia matokeo ya uchapishaji kabla ya kuchapisha kwenye CD/DVD.
(Mkao wa kuchapisha umerekebishwa)
Anza kutambaza nakala asili na uonyeshe taswira iliyotambazwa. Unaweza kurekebisha eneo la kuchapisha kwenye skrini ya uhakiki.
Rangi
Hunakili nakala asili katika rangi.
Nyeusi na Nyeupe
Hunakili nakala asili katika rangi nyeusi na nyeupe (rangi moja).
(Uzito)
Ongeza kiwango cha uzito wakati matokeo ya kunakili yamefifia. Punguza kiwango cha uzito wino unapomwagika.
Ubora
Teua ubora wa nakili. Kuteua Juu hutoa uchapishaji wa hali ya juu zaidi, lakini kasi ya uchapishaji huenda ikawa ya chini. Iwapo uanataka kuchapisha kwenye karatasi tupu ukitumia ubora wa juu zaidi, teua Bora. Kumbuka kwamba hii inaweza kupungua mno kasi ya kuchapisha.