Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Mipangilio > Mipangilio Msingi
Mipangilio Msingi
Sauti
Rekebisha sauti.
Kilezi cha Skrini
Teua Data yaKadi ya Kumbukumbu ili kuonyesha picha kama onyesho slaidi wakati hakuna operesheni zinatekelezwa kwa karibu dakika tatu.
Mwangaza wa LCD
Rekebisha mwangaza wa skrini ya LCD.
Washa Nishati Otomatiki
Teua Washa ili kuwasha kichapishi kiotomatiki kinapopokea kazi ya kuchapisha au kutambaza kupitia kwa muunganisho wa USB au muunganisho wa mtandao.
Kuwezesha Washa Nishati Otomatiki huongeza matumizi ya nishati kiasi kwenye hali ya kusubiria ikilinganishwa na kuzima kichapishi kikamilifu. Pia, inachukua muda mrefu zaidi kuzima nishati. Acha waya ya nishati ichomekwe ndani wakati unatumia kipengele hiki. Ikiwa utachomoa waya ya nishati, hakikisha mwangaza wa nishati umezimwa.
Tumia mpangilio wa Kipima Saa ya Kuzima iwapo unataka kichapishi kuzima kiotomatiki wakati kazi ya kuchapisha au kutambaza imekamilika na kipindi cha muda kilichowekwa kimepita bila operesheni kutekelezwa. Hii ni muhimu wakati uchapishaji kutoka kwa eneo la mali kama vile kupitia mtandao.
Kipima Saa ya Kuzima
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Mip'ilio ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki wakati hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Unaweza kurekebisha muda kabla ya udhibiti wa nishati kutekelezwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Mip'ilio ya Kuzima
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Kipima Saa ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Zima Ikiwa Haitumiki
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki iwapo hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Zima ikiwa Imetenganishwa
Teua mpangilio huu ili kuzima printa baada ya muda maalum wakati vituo tarishi zote ikijumuisha kituo cha USB kimetenganishwa. Kipengele hiki huenda kisipatiokane kulingana na eneo lako.
Rekebisha kipindi cha muda cha kuingia kwenye modi ya kusinzia (modi ya kuhifadhi nishati) wakati kichapishi hakijatekeleza operesheni zozote. Skrini ya LCD inakuwa nyeusi wakati muda uliowekwa unapita.
Lugha/Language
Teua lugha inayotumiwa kwenye skrini ya LCD.
Rangi ya Mandhari-nyuma
Badilisha rangi ya mandharinyuma ya skrini ya LCD.
Ondoa Mipangilio Yote
Huweka upya Mipangilio Msingi kwa chaguo-msingi yake.