Chaguo za Menyu ya Kuchapisha kutoka kwa Paneli Dhibiti
Chaguo za Menyu ya Kuchapisha kutoka kwa Paneli Dhibiti
Chaguo za Menyu za Kuteua Picha
Vinjari
Huonyesha picha kwenye kifaa cha kumbukumbu kilichopangwa kutumia masharti bainifu. Chaguo zinazopatikana kulingana na vipengele kutumiwa.
Katisha Kuvinjari:
Hukatisha upangaji wa picha na kuonyesha picha zote.
mm:
Teua mwaka wa picha unazotaka kuonyesha.
mmmm/mm:
Teua mwaka na mwezi wa picha unazotaka kuonyesha.
mmmm/mm/ss:
Teua mwaka na mwezi na tarehe ya picha unazotaka kuonyesha.
Mpangilio wa Kuonyesha
Hubadilisha mpangilio wa kuonyesha wa picha katika mpangilio wa kutoka chini hadi juu au kutoka juu hadi chini.
Teua picha zote
Huteua picha zote na kuweka idadi cha vichapisho.
Batilisha uteuzi wa picha zote
Hurudisha idadi ya machapisho ya picha zote kwa 0 (sufuri).
Chagua kifaa cha kumbukumbu
Teua kifaa ambacho unachotaka kupakia picha.
Chaguo za Menyu ya Mipangilio ya Karatasi na Chapisho
Mipangilio ya K'si
Chagua chanzo cha karatasi ambacho unataka kutumia. Chagua ili kuchagua ukubwa na aina ya karatasi.
Mpangilio wa Mpaka
Isiyo na mipaka:
Huchapisha bila pambizo kwenye kingo. Hukuzwa kiasi kidogo zaidi ya ukubwa wa karatasi ili kusiwe na pambizo zinachapishwa kando ya kingo za karatasi.
Na mipaka:
Huchapisha na pambizo nyeupe kwenye kingo.
Upanuzi
Kwa uchapishaji usio na mpaka, taswira inakuzwa kiasi ili kuondoa mipaka kutoka kwa kingo za karatasi. Teua kiwango cha kukuza taswira.
Tosheza Fremu
Ikiwa mgao uwiano wa data ya picha na ukubwa wa karatasi ni tofauti, picha hupanuliwa au kupunguzwa kiotomatiki ili pande zile fupi zilingane na pande fupi za karatasi. Upande mrefu wa picha hukatwa ikiwa unazidi upande mrefu wa karatasi. Huenda kipengele hiki kisitumike kwa picha za panorama.
Ubora
Teua ubora wa kuchapisha. Kuteua Juu hutoa uchapishaji wa hali ya juu zaidi, lakini kasi ya uchapishaji huenda ikawa ya chini. Iwapo uanataka kuchapisha kwenye karatasi tupu ukitumia ubora wa juu zaidi, teua Bora. Kumbuka kwamba hii inaweza kupungua mno kasi ya kuchapisha.
Tarehe
Chagua umbizo linalotumiwa kuchapisha tarehe kwenye picha kwa picha ambazo zinajumuisha tarehe ambayo picha ilipigwa au tarehe picha hizo zilihifadhiwa. Tarehe haichapishwi kwa baadhi ya miundo.
Mae. Kuchapisha. Kwe. Picha
Zima:
Huchapisha bila maelezo yoyote.
Mipangilio ya Kamera:
Huchapisha pamoja na baadhi maelezo ya Exif, kama vile kasi ya kupiga picha, uwiano wa f, au unyeti wa ISO. Maelezo yasiyorekodiwa hayachapishwi.
Matini ya Kamera:
Huchapisha seti ya matini kwenye kamera ya dijitali. Kwa maelezo kuhusu mipangilio ya matini, tazama nyaraka iliyotolewa kwa kamera yako. Maelezo yanaweza kuchapishwa kwenye uchapishaji usio na mpaka pekee katika ukubwa wa upana wa 10×15 cm, 13×18 cm, au 16:9.
Alamardhi:
Huchapisha jina la eneo au alamardhi ambapo picha zilichukuliwa kwa kamera za dijitali ambazo zina kipengele cha alamardhi. Tazama tovuti ya mtengenezaji wa kamera yako kwa maelezo zaidi. Maelezo yanaweza kuchapishwa kwenye uchapishaji usio na mpaka pekee katika ukubwa wa upana wa 10×15 cm, 13×18 cm, au 16:9.
Ondoa Mipangilio Yote
Rejesha mipangilio ya karatasi na uchapishaji kuwa chaguomsingi.
Uzito wa CD
Kwa uchapishaji wa CD/DVD. Weka uzito ili kutumia wakati wa kuchapisha kwenye CD/DVD.
Wiani
Kwa uchapishaji wa kitabu cha rangi. Teua kiwango cha uzito kwa ufafanuzi kwenye laha la rangi.
Ugunduaji Mstari
Kwa uchapishaji wa kitabu cha rangi. Teua uzito wa kutumia kuteua ufafanuzi kwenye picha.
Chaguo za Menyu za Kuhariri Picha
Kuza/Zungusha
Hurekebisha eneo la kupogoa. Unaweza kusogeza fremu katika eneo unalotaka kupogoa, au badilisha ukubwa wa fremu kwa kutelezesha katika pembe. Pia unaweza kuzungusha fremu.
Kichujio
Uchapishaji katika sepia au monokromu.
Boresha
Teua mojawapo ya chaguo za kurekebisha picha. Otomatiki, Watu, Mandhari, au Mandhari Usiku hutoa taswira iliyoimarika zaidi na rangi kolezwa zaidi kwa kurekebisha ulinganisho, uenevu na ung’avu wa data ya taswira asili kiotomatiki.
Otomatiki:
Kichapishi hutambua maudhui ya taswira na kuboresha taswira kiotomatiki kulingana na maudhui yaliyotambuliwa.
Watu:
Inapendekezwa kwa taswira za watu.
Mandhari:
Imependekezwa kwa taswira au mandhari.
Mandhari Usiku:
Imependekezwa kwa taswira au mandhari ya usiku.
Ub'aji Umezimwa:
Huzima kipengele cha Boresha.
Ta. Jicho Ny'u
Hurekebisha jicho jekundu kwenye picha. Marekebisho hayatekelezwi kwenye faili asili, kwenye machapisho tu. Kwa kutegemea aina ya picha, sehemy za picha kando na macho zinaweza kurekebishwa.
Ung’avu
Rekebisha ung’avu wa taswira.
Ulinganuzi
Hurekebisha tofauti kati ya mwangaza na giza.
Ukali
Huboresha au kuondoa ulengaji wa muhtasari wa taswira.