> Mahali pa Kupata Msaada > Kuwasiliana na Usaidizi wa Epson > Kabla ya Kuwasiliana na Epson

Kabla ya Kuwasiliana na Epson

Ikiwa bidhaa yako ya Epson haifanyi kazi ipasavyo na huwezi kutatua shida hiyo ukitumia taarifa ya usuluhishaji iliyo katika miongozo ya bidhaa yako, wasiliana na huduma ya usaidizi ya Epson kwa usaidizi. Ikiwa usaidizi wa Epson wa eneo lako haujaorodheshwa hapa chini, wasiliana na muuzaji aliyekuuzia bidhaa yako.

Usaidizi wa Epson utakusaidia haraka zaidi ukiwapa taarifa ifuatayo:

  • Nambari mfululizo ya bidhaa

    (Lebo ya nambari mfululizo huwa upande wa nyuma wa bidhaa.)

  • Modeli ya bidhaa

  • Toleo la programu ya bidhaa

    (Bofya About, Version Info, au kitufe sawa katika programu ya bidhaa.)

  • Chapa na modeli ya kompyuta yako

  • Jina na toleo la programu endeshi ya kompyuta yako

  • Majina na matoleo ya vipengele vya programu unavyotumia kwa kawaida na bidhaa yako

Kumbuka:

Kulingana na bidhaa, mipangilio ya mtandao inaweza kuhifadhiwa katika kumbukumbu ya bidhaa. Kwa sababu ya kuharibika au ukarabati wa bidhaa, mipangilio inaweza kufutika. Epson haitawajibika kwa kupotea kwa data yoyote, kwa kuakibisha au urejeshi wa mipangilio hata wakati wa muda wa udhamini. Tunapendekeza kwamba uakibishe data mwenye au uinakili.