Bainisha masafa ya chapisho. Hadi 120 mm ya kipenyo cha nje, na kiwango cha chini cha 18 mm cha kipenyo cha ndani kinaweza kubainishwa. Kulingana na mpangilio wa eneo la kichapishi, CD/DVD au trei ya CD/DVD huenda vikachafuka. Weka masafa ili kutosheleza aneo linalochapishika ya CD/DVD yako.
Teua iwapo utachapisha CD/DVD ili kuunda chapisho la jaribio kwenye karatasi tupu ya ukubwa wa A4. Unapoteua Test print on A4 paper unaweza kuangalia matokeo ya uchapishaji kabla ya kuchapisha kwenye CD/DVD.
(Mkao wa kuchapisha umerekebishwa):
Anza kutambaza nakala asili na uonyeshe taswira iliyotambazwa. Unaweza kurekebisha eneo la kuchapisha kwenye skrini ya uhakiki.
(Density):
Ongeza kiwango cha uzito + wakati matokeo ya kunakili ni hafifu. Punguza kiwango cha uzito kwa kutumia - wakati wino unamwagika.
Teua aina ya nakala yako asili. Hunakili katika ubora wa juu ili kulingana na aina ya hati halisi.