Chaguo za Menyu ya Mipangilio ya Karatasi na Chapisho

Paper Setting:

Chagua chanzo cha karatasi ambacho unataka kutumia. Chagua ili kuchagua ukubwa na aina ya karatasi.

Border Setting
  • Borderless:

    Huchapisha bila pambizo kwenye kingo. Hukuzwa kiasi kidogo zaidi ya ukubwa wa karatasi ili kusiwe na pambizo zinachapishwa kando ya kingo za karatasi.

  • With Border:

    Huchapisha na pambizo nyeupe kwenye kingo.

Expansion:

Kwa uchapishaji usio na mpaka, taswira inakuzwa kiasi ili kuondoa mipaka kutoka kwa kingo za karatasi. Teua kiwango cha kukuza taswira.

Fit Frame:

Ikiwa mgao uwiano wa data ya picha na ukubwa wa karatasi ni tofauti, picha hupanuliwa au kupunguzwa kiotomatiki ili pande zile fupi zilingane na pande fupi za karatasi. Upande mrefu wa picha hukatwa ikiwa unazidi upande mrefu wa karatasi. Huenda kipengele hiki kisitumike kwa picha za panorama.

Quality:

Teua ubora wa kuchapisha. Kuteua High hutoa uchapishaji wa hali ya juu zaidi, lakini kasi ya uchapishaji huenda ikawa ya chini. Iwapo uanataka kuchapisha kwenye karatasi tupu ukitumia ubora wa juu zaidi, teua Best. Kumbuka kwamba hii inaweza kupungua mno kasi ya kuchapisha.

Date:

Chagua umbizo linalotumiwa kuchapisha tarehe kwenye picha kwa picha ambazo zinajumuisha tarehe ambayo picha ilipigwa au tarehe picha hizo zilihifadhiwa. Tarehe haichapishwi kwa baadhi ya miundo.

Print Info On Photos
  • Off:

    Huchapisha bila maelezo yoyote.

  • Camera Settings:

    Huchapisha pamoja na baadhi maelezo ya Exif, kama vile kasi ya kupiga picha, uwiano wa f, au unyeti wa ISO. Maelezo yasiyorekodiwa hayachapishwi.

  • Camera Text:

    Huchapisha seti ya matini kwenye kamera ya dijitali. Kwa maelezo kuhusu mipangilio ya matini, tazama nyaraka iliyotolewa kwa kamera yako. Maelezo yanaweza kuchapishwa kwenye uchapishaji usio na mpaka pekee katika ukubwa wa upana wa 10×15 cm, 13×18 cm, au 16:9.

  • Landmark:

    Huchapisha jina la eneo au alamardhi ambapo picha zilichukuliwa kwa kamera za dijitali ambazo zina kipengele cha alamardhi. Tazama tovuti ya mtengenezaji wa kamera yako kwa maelezo zaidi. Maelezo yanaweza kuchapishwa kwenye uchapishaji usio na mpaka pekee katika ukubwa wa upana wa 10×15 cm, 13×18 cm, au 16:9.

Clear All Settings:

Rejesha mipangilio ya karatasi na uchapishaji kuwa chaguomsingi.

CD Density:

Kwa uchapishaji wa CD/DVD. Weka uzito ili kutumia wakati wa kuchapisha kwenye CD/DVD.

Density:

Kwa uchapishaji wa kitabu cha rangi. Teua kiwango cha uzito kwa ufafanuzi kwenye laha la rangi.

Line Detection:

Kwa uchapishaji wa kitabu cha rangi. Teua uzito wa kutumia kuteua ufafanuzi kwenye picha.