> Kuchapisha > Kuchapisha Picha > Kuchapisha Picha kutoka kwenye Kifaa cha Kumbukumbu > Kuchapisha Picha ya Ukubwa wa Kitambulisho

Kuchapisha Picha ya Ukubwa wa Kitambulisho

Unaweza kuchapisha picha za Kitambulisho kutumia data kwenye kifaa cha kumbukumbu. Nakala mbili za picha zinachapishwa katika ukubwa tofauti, 50.8×50.8 mm na 45.0×35.0 mm, kwenye ukubwa wa karatasi ya picha wa 10×15 cm (4×6 in.).

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 1 wa Karatasi

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 2 wa Karatasi

    Kupakia Karatasi katika Nafasi ya Nyuma ya Karatasi

  2. Chomeka kifaa cha kumbukumbu kwenye sloti ya kadi ya SD au kiweko cha USB cha kiolesura cha nje cha kichapishi.

    Kuingiza Kadi ya Kumbukumbu

    Kuchomeka Kifaa cha Nje cha USB

  3. Teua Print Photos kwenye paneli dhibiti.

  4. Teua Collage > Print Photo ID.

  5. Wakati ujumbe unaokuambia kuwa kupakia picha kumekamilika unaonyeshwa, teua OK.

  6. Teua .

  7. Teua picha unayotaka kuchapisha kwenye skrini ya kuteua picha, na kisha uteue Done.

    Teua Single View, kisha uteue ili kuhariri picha ikiwa ni muhimu.

    Chaguo za Menyu za Kuhariri Picha

  8. Teua Next.

  9. Weka mipangilio kwenye kichupo cha Basic Settings kisha uweke idadi ya nakala.

    Chaguo za Menyu ya Mipangilio ya Karatasi na Chapisho

  10. Teua kichupo cha Advanced Settings kisha ubadilishe mipangilio inavyohitajika.

  11. Teua kichupo cha Basic Settings, na kisha udonoe .