Hurekebisha eneo la kupogoa. Unaweza kusogeza fremu katika eneo unalotaka kupogoa, au badilisha ukubwa wa fremu kwa kutelezesha
katika pembe. Pia unaweza kuzungusha fremu.
Uchapishaji katika sepia au monokromu.
Teua mojawapo ya chaguo za kurekebisha picha. Auto, People, Landscape, au Night Scene hutoa taswira iliyoimarika zaidi na rangi kolezwa zaidi kwa kurekebisha ulinganisho, uenevu na ung’avu wa data ya taswira asili kiotomatiki.
Auto:
Kichapishi hutambua maudhui ya taswira na kuboresha taswira kiotomatiki kulingana na maudhui yaliyotambuliwa.
People:
Inapendekezwa kwa taswira za watu.
Landscape:
Imependekezwa kwa taswira au mandhari.
Night Scene:
Imependekezwa kwa taswira au mandhari ya usiku.
Enhance Off:
Huzima kipengele cha Enhance.
Hurekebisha jicho jekundu kwenye picha. Marekebisho hayatekelezwi kwenye faili asili, kwenye machapisho tu. Kwa kutegemea aina ya picha, sehemy za picha kando na macho zinaweza kurekebishwa.
Rekebisha ung’avu wa taswira.
Hurekebisha tofauti kati ya mwangaza na giza.
Huboresha au kuondoa ulengaji wa muhtasari wa taswira.
Rekebisha uwazi wa taswira.