> Kutatua Matatizo > Ni Wakati wa Kubadilisha Kibweta cha Wino > Tahadhari za Kushughulikia Kibweta cha Wino

Tahadhari za Kushughulikia Kibweta cha Wino

Kuhifadhi tahadhari kwa wino
  • Weka katriji za wino mbali na mwale wa jua wa moja kwa moja.

  • Usihifadhi katriji za wino katika halijoto za juu au zinazoganda.

  • Kwa matokeo bora, Epson inapendekeza utumie kibweta kizima cha wino kabla ya tarehe iliyochapishwa kwenye kifurushi au ndani ya miezi sita baada ya kufungua kifurushi, muda wowote unaotangulia.

  • Kwa matokeo mazuri zaidi, hifadhi pakiti za katriji za wino upande wa chini ukiwa chini.

  • Baada ya kuleta katriji ya wino ndani kutoka eneo, iwache ipate joto kwa halijoto ya chumba kwa angalau saa tatu kabla ya kuitumia.

  • Usifungue pakiti ya katrji ya wino hadi uwe tayari kuweka ndani ya printa. Katriji hupakiwa bila hewa ili kudumisha utumikaji wake. Ukiiwacha katriji ikiwa haijapakiwa kwa muda mrefu kabla ya kuitimia, uchapishaji wa kawaida huenda usiwezekane.

Tahadhari za shughuli ya kubadilisha katriji za wino
  • Usiguse sehemu zinazoonyeshwa kwenye picha. Kufanya hivyo kunaweza kuzuia utendaji na uchapishaji wa kawaida.

  • Funga katriji zote za wino; la zivyo hutaweza kuchapisha.

  • Usibadilishe katriji za wino wakati printa imezimwa. Usisogeze kichwa cha kushapisha ukitumia mkono; la sivyo unaweza kuharibu printa.

  • Baada ya kufunga kariji ya wino, taa ya nisha inaendelea kumweka wakati printa inanyonya wino. Usizime printa wakati wa kunyonya wino. Ikiwa unyonyaji wa wino haujakamilika, huwezi kuchapisha.

  • Usiache kichapishi kikiwa na katriji za wino zimeondolewa au usixzime kichapishi wakati wa kubadilisha katriji. Vinginevyo, wino unaosalia kwenye nozeli za kichwa cha kuchapisha utakauka na huenda usiweze kuchapisha.

  • Kuwa makini vumbi au vitu vingine vyovyote visiingie ndani ya kibanio cha katriji ya wino. Kitu chochote kilicho ndani ya kibanio kinawea kuathiri matokeo ya uchapishaji pakubwa au kusababisha kutoweza kuchapisha. Kitu chochote kikiingia ndani ya kibania, kiondoe kwa uangalifu.

  • Ukiondoa katriji kutoka kwa printa kwa matumizi ya baadaye au kuitumpa, hakikisha umefunika lango la kutoa wino la katriji ili kuzuia wino kukauka au kuzuia maeneo yaliyo kando yasimwagikiwe na wino.

  • Iwapo utaondoa katriji ya wino kutoka kwenye kichapisbhi kwa matumizi ya baadaye, Epson hupendekeza kuitumia haraka iwezekanavyo.

  • Printa hii hutumia katriji zilizo na chipu ya kijani inayofuatilia maelezo kama vile kiwango cha wino kinachobakia kwa kila katriji. Hii inamaanisha kwamba hata kama katriji imeondolewa kutoka kwa printa kabla ya kumalizika, bado unaweza kutumia katriji hiyo baada ya kuiingiza upya katika printa. Hata hivyo, unapoingiza katriji upya, kiasi fulani cha wino kinaweza kutumiwa ili kuhakikisha utendaji wa printa.

  • Kwa matumizi mazuri kabisa ya wino, ondoa katriji ya wino wakati uko tayari kuibadilisha peke yake. Katriji za wino zilizo na hali ya chini ya wino haziwezi kutmiwa wakati zimeingizwa upya.

  • Ili kuhakikisha unapata uchapishaji wa ubora wa juu na kusaidia kulinda kicha chako cha uchapishaji, akiba tofauti ya usalama ya wino hubakia katika katriji wakati printa yako inakuonyesha unafaa kubadilishwa katriji. Viwango vilivyoandikwa havijumuishi akiba hii.

  • Usifungue au kubadilisha modeli ya katriji ya wino, la sivyo huenda usiweze kuchapisha kwa kawaida.

  • Huwezi kutumia katriji zilizokuja na printa kufanya mabadilisho.

  • Maliza ubadilishaji wa katriji ya wino bila kuchelewa. Usiwache printa wakati katriji za wino zimeondolewa.

Matumizi ya wino
  • Ili kudumisha utendaji mzuri wa kichwa cha kuchapisha, kiasi fulani cha wino hutumiwa kutoka kwa katriji zote wakati wa operesheni za matengenezo. Huenda wino ukatumika unapobadilisha katriji za wino au kuwasha kichapishi.

  • Wakati unachapisha rangi moja au kijivujivu, wino wa rangu badala ya wino mweusi unaweza kutumiwa kulingana na aina ya karatasi au mipangilio ya ubora wa uchapishaji. Hii ni kwa sababu mchanganyiko wa wino wa rangu unatumiwa kutengeneza rangi nyeusi.

  • Wino katika katriji za wino zilizokuja na printa yako zimetumwa kwa kiasi fulani wakati wa usanidi wa mwanzo. Ili uchapishe nakala za hali ya juu, kichwa cha kuchapisha kilicho katika printa yako kitajazwa wino. Mchakato huu wa mara moja hutumia kiasi cha wino na basi katriji hizi zinaweza kuchapisha kurasa chache kulingana na katriji za wino zitakazofuata.

  • Viwango viliandikwa vinaweza kuwa tofauti kulingana na picha unazochapisha, aina ya karatasi unayotumia, marudio ya uchapishaji na hali ya mazingisa kama vile halijoto.