Angalia hitilafu inayoonyeshwa kwenye paneli dhibiti na ufuate maelekezo ili uondoe karatasi iliyokwama ikiwa ni pamoja na vipande vilivyoraruka. Bkisha, futa hitilafu. Skrini ya LCD huonyesha uhuishaji unaonkuoyesha jinsi ya kuondoa karatasi iliyokwama.
Usiwahi kugusa vitufe vilivyo kwenye paneli dhibiti wakati mkono wako uko ndani ya kichapishi. Ikiwa kichapishi kitaanza kufanya kazi, inaweza kusababisha majeraha. Kuwa makini usiguse sehemu zinazojitokeza ili uzuie majeraha.
Ondoa karatasi iliyokwama kwa uangalifu. Kuondoa karatasi kwa nguvu kunaweza kusababisha uharibifu wa printa.