Iwapo kichapishi kimeunganishwa kwenye Mtandao, unaweza kusasisha programu dhibiti ya kichapishi kwa kutumia paneli dhibiti. Kwa kusasisha programu dhibiti, utendakazi wa kichapishi unaweza kuboreka, au vitendaji vipya vinaweza kuongezezwa. Pia unaweza kuweka kichapishi katika ukaguzi wa kila mara kwa visasisho vya programu dhibiti na kukuarifu iwapo kuna vyovyote vinavyopatikana.
Teua Settings kwenye skrini ya nyumbani.
Teua Firmware Update > Update.
Wezesha Notification ili kuweka kichapishi kwa ukaguzi wa kila mara kwa visasisho vinavyopatikana vya programu dhibiti.
Angalia ujumbe unaonyeshwa kwenye skrini na uchague Start Checking.
Angalia ujumbe unaonyeshwa kwenye skrini na uchague Start.
Programu dhibiti imesasishwa wakati programu dhibiti mpya imepatikana. Pindi tu usasishaji ukianza, hauwezi kukatishwa.
Usizime au kuchomoa kichapishi hadi usasishaji ukamilike. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha kichapishi kutofanya kazi.
Iwapo programu dhibiti haijakamilika au haijafanikiwa, kichapishi hakitaanza kazi kwa nja ya kawaida na “Recovery Mode” inaonyeshwa kwenye skrini ya LCD wakati mwingine kichapishi kitakapowashwa. Katika hali hii, unahitaji kusasisha tena programu dhibiti kwa kutumia kompyuta. Unganisha kichapishi kwenye kompyuta kwa kebo ya USB. Wakati “Recovery Mode” inaonyeshwa kwenye kichapishi, huwezi kusasisha programu dhibiti kupitia muunganisho wa mtandao. Kwenye kompyuta, fikia tovuti yako ya ndani ya Epson, na kisha upakue programu dhibiti ya sasa ya kichapishi. Tazama maagizo kwenye tovuti kwa hatua zifuatazo.