> Utambazaji > Utambazaji wa Kina > Kutambaza Picha nyingi kwa Wakati Mmoja

Kutambaza Picha nyingi kwa Wakati Mmoja

Ukitumia Epson ScanSmart, unaweza kutambaza picha nyingi kwa wakati mmoja na kuhifadhi kila moja peke yake.

  1. Weka picha kwenye glasi ya kichanganuzi. Ziweke kwa umbali wa 4.5 mm (0.2 in) mbali na kingo za mlalo na wima za glasi ya kitambazaji, na uzitengenishe kwa umbali wa angalau 20 mm (0.8 in.).

    Kumbuka:

    Picha zinapaswa kuwa kubwa kuliko 15×15 mm (0.6×0.6 in.).

  2. Anzisha Epson ScanSmart.

    • Windows 10
      Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Epson Software > Epson ScanSmart.
    • Windows 8.1/Windows 8
      Andika jina la programu katika sehemu ya utafutaji, na kisha uchague ikoni inayoonekana.
    • Windows 7
      Bofya kitufe cha kuwasha kisha uteue Programu Zote > Epson Software > Epson ScanSmart.
    • Mac OS
      Teua Nenda > Programu > Epson Software > Epson ScanSmart.
  3. Wakati skrini ya Epson ScanSmart inaonyeshwa, fuata maelekezo kwenye skrini ili kutambaza.

Picha zilizotambazwa huhifadhiwa kama picha binafsi.