> Kuchapisha > Kuchapisha Picha > Kuchapisha Picha kutoka kwenye Kifaa cha Kumbukumbu > Kuchapisha Mkusanyiko wa Picha na Ruwaza za Mandharinyuma

Kuchapisha Mkusanyiko wa Picha na Ruwaza za Mandharinyuma

Unaweza kuchapisha picha kwenye kifaa cha kumbukumbu kwa kuunda mpangilio na kuongeza ruwaza ya mandharinyuma.

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 1 wa Karatasi

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 2 wa Karatasi

    Kupakia Karatasi katika Nafasi ya Nyuma ya Karatasi

  2. Chomeka kifaa cha kumbukumbu kwenye sloti ya kadi ya SD au kiweko cha USB cha kiolesura cha nje cha kichapishi.

    Kuingiza Kadi ya Kumbukumbu

    Kuchomeka Kifaa cha Nje cha USB

  3. Teua Print Photos kwenye paneli dhibiti.

  4. Teua Collage > Photo Collage.

  5. Teua mpangilio.

  6. Chagua aina ya mandharinyuma unayotaka kutumia. Huenda hii isipatikane kwa baadhi ya mipangilio.

    • Design
      Teua ruwaza, kama vile mipaka au nukta polka au Original Design kisha uteue ruwaza uliyounda kwa kutumia kipengele cha ruwaza ya karatasi.
    • No Background
      Nenda kwa hatua inayofuata.
  7. Wakati ujumbe unaokuambia kuwa kupakia picha kumekamilika unaonyeshwa, teua OK.

  8. Fanya moja kati ya zifuatazo.

    • Unapoteua mpangilio wa picha moja katika hatua ya 5: Teua , teua picha moja kwenye skrini ya picha kisha uteue Next. Nenda kwenye hatua ya 13.
    • Unapoteua mpangilio wa picha nyingi katika hatua ya 5 na kuweka picha kiotomatiki: Teua Automatic Layout, teua picha kwenye skrini ya kuteua picha kisha uteue Next. Nenda kwenye hatua ya 13.
    • Unapoteua mpangilio wa picha nyingi na kuweka picha mwenyewe: Nenda katika hatua inayofuata.
  9. Teua .

  10. Teua picha unayotaka kuchapisha kwenye skrini ya kuteua picha, na kisha uteue Done.

    Teua Single View, kisha uteue ili kuhariri picha ikiwa ni muhimu.

    Chaguo za Menyu za Kuhariri Picha

  11. Rudia hatua za 9 hadi 10 hadi picha zote ziwekwe.

  12. Teua Next.

  13. Weka mipangilio kwenye kichupo cha Basic Settings kisha uweke idadi ya nakala.

    Chaguo za Menyu ya Mipangilio ya Karatasi na Chapisho

  14. Teua kichupo cha Advanced Settings kisha ubadilishe mipangilio inavyohitajika.

  15. Teua kichupo cha Basic Settings, na kisha udonoe .