Mkao wa Kunakili kwenye CD/DVD si sahihi

Sababu zifuatazo zinaweza kuzingatiwa.

Sehemu ya kuchapisha inahitaji kurekebishwa.

Suluhisho

Teua menyu ya Settings > Printer Settings > CD/DVD kwenye paneli dhibiti na urekebishe sehemu ya uchapishaji.

Kuna vumbi au uchafu kwenye glasi ya kichanganuzi.

Suluhisho

Safisha glasi ya kichanganuzi na kifuniko cha waraka ukitumia nguo kavu, laini na safi. Iwapo kuna vumbi au uchafu pembeni mwa glasi, eneo la nakala linaweza kusambaa na kujumuisha vumbi au uchafu na kusababisha nafasi isiyo sahihi ya kunakili au taswira ndogo.