> Kuhifadhi na Kushiriki Data > Kushiri Data kwenye Kifaa cha Kumbukumbu

Kushiri Data kwenye Kifaa cha Kumbukumbu

Kutoka kwenye kompyuta, unaweza kuandika au kusoma data kwenye kifaa cha kumbukumbu kama vile kadi ya kumbukumbu ambayo imechomekwa kwenye kichapishi.

Muhimu:
  • Chomeka kadi ya kumbukumbu baada ya kuondoa ulinzi wa kuandika.

  • Iwapo taswira imehifadhiwa kwenye kadi ya kumbukumbu kutoka kwenye kompyuta, taswira na idadi ya picha hazionyeshiw upya kwenye skrini ya LCD. Ondoa na uchomeke tena kadi ya kumbukumbu.

  • Unaposhiriki kifaa cha kumbukumbu kilichochomekwa kwenye kichapishi kati ya kompyuta iliyounganishwa na USB au kupitia mtandao, haki ya ufikiaji imeruhusiwa tu kwa kompyuta zimeunganishwa kupitia mbinu ambayo uliteua kwenye kichapishi. Ili kuandika kwenye kifaa cha kumbukumbu, weka Settings kwenye paneli dhibiti, kisha uteue File Sharing Setup na mbinu ya muunganisho.

Kumbuka:

Huchukua muda ili kutambua data kutoka katika kompyuta ikiwa kifaa kikubwa cha kumbukumbu kama vile TB 2 HDD kimeunganishwa.

Windows

Teua kifaa cha kumbukumbu kutoka Kompyuta au Kopmyuta Yangu. Data kwenye kifaa cha kumbukumbu inaonyeshwa.

Kumbuka:

Ikiwa umeunganisha printa kwenye mtandao bila diski ya programu au Web Installer, kuweka nafasi ya kadi ya kumbukumbu au kituo cha USB kama kiendeshi cha mtandao. Fungua Endesha na uingize jina la kichapishi \\XXXXX au anwani ya IP ya kichapishi \\XXX.XXX.XXX.XXX ili Fungua:. Bofya kulia kwenye ikoni ya kifaa iliyoonyeshwa ili upangie mtandao. Kiendeshi cha mtandao hutokea katika Kompyuta au Kompyuta Yangu.

Mac OS

Teua ikoni inayolingana ya kifaa. Data kwenye kifaa cha hifadhi ya nje inaonyeshwa.

Kumbuka:
  • Ili kuondoa kifaa cha kumbukumbu, buruta na udondoshe aikoni ya kifaa kwenye aikoni ya tupio. Vinginevyo, huenda data kwenye hifadhi ya pamoja isionyeshwe ipasavyo wakati kifaa kingine cha kumbukumbu kimechomekwa.

  • Ili kufikia kifaa cha kumbukumbu kupitia mtandao, teua, Nenda > Unganisha kwenye Seva kutoka katika menyu kwenye eneo-kazi. Ingiza jina la kichapishi cifs://XXXXX au smb://XXXXX (Ambapo “XXXXX” ni jina la kichapishi) katika Anwani ya Seva, na kisha ubofye Unganisha.