> Kupakia Karatasi na CD/DVD > Kuweka Karatasi > Kupakia Karatasi > Kupakia Karatasi katika Nafasi ya Nyuma ya Karatasi

Kupakia Karatasi katika Nafasi ya Nyuma ya Karatasi

Muhimu:

Usipakie karatasi katika nafasi ya nyuma ya karatasi hadi printa ikuulize ufanya hivyo. Kufanya hivyo kutasbabisha karatasi tupu kutemwa.

  1. Fanya moja kati ya zifuatazo.

    • Unapochapisha kutoka kwenye paneli dhibiti: Teua nafasi ya nyuma ya karatasi kama Paper Setting, weka mipangilio mingine ya uchapishaji kisha udonoe .
    • Unapochapisha kutoka kwenye kompyuta: Teua nafasi ya nyuma ya karatasi kama mipangilio ya Chanzo cha K'tasi, weka mipangilio mingine ya uchapishaji kisha ubofye Chapisha.
  2. Ujumbe unaonyeshwa kwenye paneli dhibiti unaokuambia kuwa kichapishi kinajitayarisha, na kisha unaagizwa kupakia karatasi.

  3. Fungua kifuniko cha nafasi ya nyuma ya karatasi.

  4. Telezesha nje auni ya karatasi na upindue auni nyuma hadi iingie mahali pake.

  5. Telezesha nje miongozo ya kingo.

  6. Pakia laha moja la karatasi katikati ya nafasi ya nyuma ya karatasi na upande unaoweza kuchapishwa ukiangalia juu, na kisha uichomeke kwa takriban 5 cm kwenye kichapishi.

  7. Telezesha miongozo ya kingo kwenye ukingo wa karatasi.

  8. Donoa ili kuanza kuchapisha.