> Kutatua Matatizo > Ni wakati wa Kubadilisha Kikasha cha Matengenezo > Kubadilisha Kisanduku cha Ukarabati

Kubadilisha Kisanduku cha Ukarabati

Katika mizunguko fulani ya uchapishaji viango vidogo vya wino wa ziada vinaweza kukusanywa katika kisanduku cha ukarabati. Ili uzuie uvujaji wa wino kutoka kwa kisanduku cha ukarabati, printa imeundwa kusimamisha uchapishaji wakati uwezo wa kunyonya wa kisanduku cha ukarabati imefikisha kikomo chake. Kuhitajika kwake na mara inayohitajika kutatofautiana kulingana na idadi ya kurasa unazochapisha, aina ya nyenzo unayochapisha na idadi ya mizunguko ya usafisha ambayo printa inafanya. Wakati ujumbe unaonyeshwa ukikustua kubadilisha kisanduku cha ukarabati, anadaa bisibisi yenye kichwa tambarare na ufuate maagizo ya kwenye skrini. Kuhitajika kwa ubadilishaji wa kisanduku hakumaanishi kwamba printa yako imewacha kufanya kazi kulingana na sifa zake. Udhamini wa Epson hausimamii gharama ya ubadilishaji huu. Ni sehemu inayokarabatiwa na mtumiaji.

Kumbuka:
  • Wakati kikasha cha matengenezo kimejaa, huwezi kuchapisha au kusafisha kichwa cha kuchapisha hadi kibadilishwe ili kuzuia umwagikaji wa wino. Hata hivyo, unaweza kutenda shughuli zisizotumia wino kama vile utambazaji.

  • Wakati skrini inayofuata imeonyeshwa, sehemu haiwezi kubadilishwa na watumiaji. Wasiliana na usaidizi wa Epson.

    Uchapishaji usiokuwa na mpaka haupatikani, lakini kuchapisha mpaka kunapatikana.

  1. Ondoa kisanduku kipya cha ukarabati kutoka kwa kifurushi chake.

    Muhimu:

    Usiguse chipu ya kijani iliyo upande wa kando wa kisanduku cha ukarabati. Kufanya hivyo kunaweza kuzuia utendaji na uchapishaji wa kawaida.

    Kumbuka:

    Mfuko angavu wa kisanduku kilichotumika cha ukarabati umetolewa pamoja na kisanduku kipya cha ukarabati.

  2. Fungua kifuniko cha hati.

  3. Fungua paneli dhibiti.

  4. Fungua skuru kwa kiingiza skuru ukitumia bisibisi tambarare hadi kifuniko cha kikasha cha matengenezo king’oke kutoka kwenye kichapishi.

  5. Ondoa kifuniko cha kikasha cha matengenezo.

  6. Ondoa kisanduku kilichotumika cha ukarabati.

    Muhimu:

    Usiguse sehemu zinazoonyeshwa kwenye picha. Ukifanya hivyo unaweza kuzuia utendaji wa kawaida na unaweza kujipaka wino.

  7. Weka kisanduku kilichotumika cha ukarabati katika mfuko angavu ambao ulikuwa pamoja na kisanduku kipya cha ukarabati na ufungu mfuko huo.

  8. Ingiza kisanduku kipya cha ukarabati ndani ya printa.

  9. Weka upya kifuniko.

    Muhimu:

    Chomeka vichupo kwenye sloti, na kisha ukaze parafujo. Iwapo kifuniko hakijasakinishwa sahihi, wino unaweza kuvuja.

  10. Funga kifuniko cha hati.

  11. Teua Done.

    Muhimu:

    Iwapo kisanduku cha ukarabati hakiwezi kutambuliwa, jaribu kukisakinisha tena. Iwapo bado hakitambuliki, badilisha kisanduku cha ukarabati. Pindi tu baada ya kusakinisha kisanduku cha ukarabati kwenye kichapishi maalum hakiwezi kutumika kwa vichapishi vingine.