Unaweza kuchapisha picha pasi waya kutoka kwa kamera za dijitali zinazoauni DPS kupitia viwango vya IP (kutoka hapa inayojulikana kama PictBridge (LAN ya pasi waya)).
Hakikisha ikoni inayoonyesha kuwa kichapishi kimeunganishwa kwenye mtandao wa pasi waya ulioonyeshwa kwenye skrini ya nyumbani.
Pakia karatasi katika kichapishi.
Kupakia Karatasi katika Mkanda 1 wa Karatasi
Teua Settings > Camera Print Settings kwenye paneli dhibiti.
Teua Print Settings au Photo Adjustments na ubadilishe mipangilio iwapo ni muhimu.
Unganisha kamera ya dijitali kwenye mtandao sawa kama kichapishi.
Onyesha orodha ya vichapishi vinavyopatikana kwenye kamera ya dijitali, na kisha uteue kichapishi unachotaka kuunganishwa kwao.
Ili kuangalia jina la kichapishi, donoa ikoni ya hali ya mtandao kwenye skrini ya nyumbani.
Iwapo kamera yako ya dijitali ina kitendaji ambacho hukuruhusu kusajili vichapishi, unaweza kuunganisha kwenye kichapishi kwa kuiteua kutoka wakati unaofuata.
Teua picha unazotaka kuchapisha kutoka kwa kamera ya dijitali, unda mipangilio kama idadi ya nakala, na kisha uanze kuchapisha.
Tenganisha muunganisho wa PictBridge (LAN ya pasi waya) kwenye kichapishi kutoka kwa kamera ya dijitali.
Unapotumia PictBridge (LAN ya pasi waya), huwezi kutumia vitandaji vya kichapishi kingine au chapisho kutoka kwa vifaa vingine. Tenganisha mara moja unapokamilisha kuchapisha.