> Utambazaji > Maelezo Msingi kuhusu Utambazaji > Matumizi ya Utambazaji

Matumizi ya Utambazaji

Unaweza kutumia utambazaji kwa njia mbalimbali ili kufanya maisha kuwa rahisi zaidi.

  • Kwa kutambaza waraka wa karatasi na kuigueza kuwa data ya kidjitali, unaweza kuisoma kwenye kompyuta ai kifaa maizi.

  • Kwa kutambaza tiketi au mabngo kuwa data ya kidijitali, unaweza kutupa nakala asili na kupunguza mrundiko.

  • Kwa kutambaza nyaraka muhimu, unaweza kuweka nakala rudufu kwenye huduma ya wingu au midia nyingine ya uhifadhi, uzipate endapo zitapotea.

  • Unaweza kutuma picha au nayaraka zilizotambazwa kwa marafiki kupitaia barua pepe.

  • Kwa kutambaza ufafanuzi uliochorwa kwa mikono na kadhalika, unaweza kuushiriki kwenye mitandao ya kijamii katika ubora wa juu zaidi kuliko kupiga tu picha kwenye kifaa chako maizi.

  • Kwa kutambaza kurasa zako unazopenda kutoka magazeti au jarida, unaweza kuzihifadhi na kisha kutupa nakala asili.