> Kuchapisha > Kuchapisha Nyaraka > Kuchapisha Nyaraka kutoka Vifaa Maizi (Android) > Kuchapisha Nyaraka Ukitumia Epson iPrint

Kuchapisha Nyaraka Ukitumia Epson iPrint

Kumbuka:

Uendeshaji unaweza kutofautiana kulingana na kifaa.

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 1 wa Karatasi

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 2 wa Karatasi

    Kupakia Karatasi katika Nafasi ya Nyuma ya Karatasi

  2. Sanidi kichapishi chako kwa uchapishi wa pasi waya.

  3. Ikiwa Epson iPrint haijasakinishwa, isakinishe.

    Kusakinisha Epson iPrint

  4. Unganisha kifaa chako maizi kwenye mtandao pasiwaya kilipounganishwa kichapishi chako.

  5. Anzisha Epson iPrint.

  6. Donoa Document kwenye skrini ya nyumbani.

  7. Donoa mahali pa waraka unapiotaka kuchapisha.

  8. Teua waraka kisha udonoe Next.

  9. Donoa Print.