> Mwongozo wa Paneli Dhibiti > Usanidi wa Skrini ya Nyumbani

Usanidi wa Skrini ya Nyumbani

Huonyesha skrini ya Supply Status.

Unaweza kuangalia kiwango cha wino na kiwango cha maisha ya huduma ya kikasha cha ukarabati. Unaweza kubadilisha kibweta cha wino au uchapishe hali ya laha iliyowekwa.

Huonyesha hali ya muunganisho wa mtandao. Angalia yafuatayo kwa maelezo zaidi.

Mwongozo kwa Aikoni ya Mtandao

Huonyesha kuwa Quiet Mode imewekwa klwa kichapishi. Kipengele kinapowezeshwa, kelele iliyopigwa na operesheni za kichapishi inapunguika, lakini kasi ya kuchapisha inaweza kupungua. Hata hivyo, huenda kelele isipungue kwenye aina ya karatasi iliyoteuliwa na ubora wa chapisho. Donoa ili kubadilisha mpangilio. Unaweza pia kuweka mipangilio hii kutoka kwenye menyu ya Settings.

Settings > Printer Settings > Quiet Mode

Huonyesha skrini ya Help. Unaweza kutazama maagizo ya kuendesha au utatuzi wa matatizo.

Huonyesha kila menyu.

  • Copy

    Hukuruhusu kunakili nyaraka na picha.

  • Print Photos

    Hukuruhusu kuchapisha picha kwenye kifaa cha kumbukumbu kama vile kadi ya kumbukumbu au hifadhi ya USB.

  • Scan

    Hukuruhusu kutambaza nyaraka au picha na kuzihifadhi kwenye kifaa cha kumbukumbu au kompyuta.

  • Various Prints

    Hukuruhusu kutoa nakala kadhaa na kuchapisha karatasi undwa au vipengee mbalimbali vya nakala asili.

  • Settings

    Hukuruhusu kuweka mipangilio inayohusiana na udumishaji, mipangilio ya kichapishi na operesheni.

  • Maintenance

    Huonyesha menyu zinazopendekezwa kuimarisha ubora wa machapisho yako kama vile kuzibua nozeli kwa kuchapisha ruwaza ya ukaguaji nozeli na kutekeleza usafishaji wa kichwa, na kuboresha ukungu au mistari kwenye machapisho yako kwa kupangilia kichwa cha kuchapisha.

  • Smartphone connect

    Huonyesha menyu ili kuunganisha kichapishi kwenye kifaa maizi au kompyuta yako ndogo.

Hutelezesha skrini upande wa kulia.

Huhifadhi trei towe.