Unaweza kuchapisha picha kwenye kifaa cha kumbukumbu kwa matini au michoro iliyoandikwa kwa mkono. Hii hukuruhusu kuunda kadi asili kama vile kadi za Mwaka Mpya au kadi za siku ya kuzaliwa.
Kwanza teua picha na uchapishe kiolezo kwenye karatasi tupu. Andika au chora kwenye kiolezo na kisha ukitambaze kwa kichapishi. Kisha unaweza kuchapisha picha kwa madokezo na michoro yako ya binafsi.

Chomeka kifaa cha kumbukumbu kwenye sloti ya kadi ya SD au kiweko cha USB cha kiolesura cha nje cha kichapishi.
Kuchomeka Kifaa cha Nje cha USB
Usiondoe kifaa cha kumbukumbu hadi umalize kuchapisha.
Teua Various Prints kwenye paneli dhibiti.
Teua Greeting Card > Select Photo and Print Template.
Wakati ujumbe unaokuambia kuwa kupakia picha kumekamilika unaonyeshwa, teua OK.
Teua picha unayotaka kuchapisha kwenye skrini ya kuteua picha, na kisha uteue Next.
Kuweka mipangilio ya chapisho kama vile aina ya karatasi au muundo wa kuchapisha picha yenye madokezo yaliyoandikwa kwa mkono, kisha kuchagua Select Photo and Print Template.
Pakia karatasi tupu ya ukubwa wa A4 kwenye mkanda 2 wa karatasi ili kuchapisha kiolezo.
Donoa
ili kuchapisha kiolezo.
Angalia chapisho, na kisha uteue Close.
Fuata maagizo kwenye kiolezo ili kuandika na kuchora.
Fungua trei ya towe. Pakia karatasi ya picha kwenye mkanda 1 wa karatasi.
Teua Print Using the Template.
Chagua How To, kisha uweke kiolezo kwenye glasi ya kichanganuzi.
Hakikisha kuwa matini kwenye kiolezo yamekauka kabisa kabla ya kukiweka kwenye glasi ya kichanganuzi. Ikiwa kuna madoa kwenye glasi ya kichanganuzi, madoa hayo pia huchapishwa kwenye picha.
Chagua Edit ili kubadilisha picha ikiwa ni muhimu.
Ingiza idadi ya nakala, na kisha udonoe
.