Kulinganisha Kichwa cha Kuchapisha

Ukiona kutolingana kwa mistari wima au picha zenye ukungu, linganisha kichwa cha kuchapisha.

  1. Pakia karatasi ya ukubwa wa A4 kwenye kichapishi.

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 2 wa Karatasi

  2. Teua Maintenance kwenye skrini ya nyumbani.

  3. Teua Print Head Alignment.

  4. Teua mojawapo ya menyu za kupangilia.

    • Vertical Alignment: Chagua hii ikiwa uchapishaji wako utaonekana ukiwa na ukungu au mistari isiyolingana.
    • Horizontal Alignment: Chagua hii ikiwa utaona mistari mlalo mara kwa mara.
  5. Fuata maagizo ya kwenye skrini na ruwaza ya kupangilia na kuteua nambari kwa ruwaza nzuri.

    • Vertical Alignment: Tafuta na uteue nambari ya ruwaza imara zaidi katika kila kundi.
    • Horizontal Alignment: Tafuta na uteue nambari ya ruwaza iliyogawanywa na inayopindana.