> Kunakili > Kunakili Nakala Asili > Kunakili kwa Kupanua au Kupunguza

Kunakili kwa Kupanua au Kupunguza

Unaweza kunakili nakala asili kwa upanuzi uliobainishwa.

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 1 wa Karatasi

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 2 wa Karatasi

    Kupakia Karatasi katika Nafasi ya Nyuma ya Karatasi

  2. Weka nakala za kwanza.

    Kuweka nakala Asili kwenye glasi ya kichanganuzi

  3. Teua Copy kwenye paneli dhibiti.

  4. Teua kichupo cha Copy, na kisha ubadilishe mipangilio kama inavyohitajika.

    Chaguo za Menyu kwa Kunakili

  5. Teua kichupo cha Advanced Settings, na kisha uteue Reduce/Enlarge.

  6. Bainisha ukubwa ili kulingana na ukubwa wa nakala asili na ukubwa wa karatasi ulioweka, kisha uteue OK.

    Iwapo umeteua Auto Fit Page, hugundua sehemu ya kutambaza kiotomatiki na kupanua au kupunguza nakala asili kulingana na ukubwa wa karatasi uliyoteua.

  7. Badilisha mipangilio mingine inavyohitajika.

    Chaguo za Menyu kwa Kunakili

  8. Teua kichupo cha Copy, na kisha uweke idadi ya nakala.

  9. Donoa .

    Kumbuka:
    • Iwapo utateua Preview, unaweza kuangalia taswira zilizotambazwa.

    • Rangi, ukubwa, na ukingo wa taswira iliyonakiliwa ni tofauti kiasi kutoka kwenye nakala asili.