Kwa kutumia Epson Event Manager, unaweza kuweka Follow custom setting ya kutambaza kwa kompyuta kwa kutumia paneli dhibiti.
Angalia msaada wa Epson Event Manager ili upate maelezo.
Anzisha Epson Event Manager.
Hakikisha kuwa kitambazaji chako kimeteuliwa kama Scanner kwenye kichupo cha Button Settings katika skrini kuu.

Bofya Make Job Settings.

Weka mipangilio kutambaza kwenye skrini ya Job Settings.

Bofya OK ili kurudi kwenye skrini kuu.
Hakikisha kuwa Custom Action imeteuliwa kwenye orodha ya Custom Action.

Bofya Close ili kufunga Epson Event Manager.