Huchapisha ruwaza ya ukaguaji nozeli ili kuangalia iwapo nozeli za kichwa cha kuchapisha zimeziba.
Husafisha nozeli zilizoziba katika kichwa cha kuchapisha. Kwa sababu kipengele hiki hutumia wino, safisha kichwa cha kuchapisha tu iwapo nozeli zimeziba. Chapisha ruwaza ya ukaguaji nozeli kisha uteue Inasafisha ikiwa kuna matatizo machache tu kwenye ruwaza. Usafishaji wa Nishati hutumia wino mwingi kuliko Inasafisha. Tumia hii tu ikiwa kuna matatizo mengi katika ruwaza ya kukagua nozeli.
Kipengele cha Job Arranger Lite hukuruhusu kujumuisha faili mbalimbali zilizoundwa na programu tofuti na uzichapishe kama kazi moja ya uchapishaji.
Hufungua dirisha la EPSON Status Monitor 3. Unaweza kuthibitisha hali ya kichapishi na matumizi yake hapa.
Hukuruhusu kuunda mipangilio kwa vipengee kwenye dirisha la EPSON Status Monitor 3.
Hukuruhusu kuunda mipangilio mbalimbali. Bofya kulia kila kipengee ili kuona Msaada kwa maelezo zaidi.
Huonyesha kazi zinazosubiri kuchapishwa. Unaweza kuangalia, kusitisha, au kuendelea na kazi za kuchapisha.
Hubadilisha lugha ya kutumiwa kwenye dirisha la kiendeshi cha kichapishi. Ili kutekeleza mipangilio, funga kiendeshi cha kichapishi, na kisha ukifungue tena.