> Kuchapisha > Kuchapisha Picha > Kuchapisha Picha kutoka kwenye Kifaa cha Kumbukumbu > Kuchapisha Picha kwenye Jaketi ya Kasha la Kito

Kuchapisha Picha kwenye Jaketi ya Kasha la Kito

Unaweza kuchapisha picha kwenye jaketi ya kasha la kito kwa urahisi kutumia picha iliyo kwenye kifaa chako cha kumbukumbu. Chapisha jaketi kwenye karatasi ya ukubwa wa A4, na kisha uikate ili kuitosheleza kwenye kasha la kito.

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 2 wa Karatasi

  2. Chomeka kifaa cha kumbukumbu kwenye sloti ya kadi ya SD au kiweko cha USB cha kiolesura cha nje cha kichapishi.

    Kuingiza Kadi ya Kumbukumbu

    Kuchomeka Kifaa cha Nje cha USB

  3. Teua Various Prints kwenye paneli dhibiti.

  4. Teua Copy to CD/DVD > Print on Jewel Case.

  5. Teua mpangilio.

  6. Wakati ujumbe unaokuambia kuwa kupakia picha kumekamilika unaonyeshwa, teua OK.

  7. Fanya moja kati ya zifuatazo.

    • Ukiteua Jewel Upper katika hatua ya 5: Teua , teua picha moja kwenye skrini ya picha, kisha uteue Done. Teua Next.
    • Ukiteua Jewel Index katika hatua ya 5: Teua picha hadi idadi ya picha unazoweza kuweka iwe 0, kisha uteue Next.

    Teua Single View, kisha uteue ili kuhariri picha ikiwa ni muhimu.

    Chaguo za Menyu za Kuhariri Picha

  8. Weka mipangilio kwenye kichupo cha Basic Settings.

    Chaguo za Menyu ya Mipangilio ya Karatasi na Chapisho

  9. Teua kichupo cha Advanced Settings kisha ubadilishe mipangilio inavyohitajika.

  10. Teua kichupo cha Basic Settings, na kisha udonoe .