> Kuchapisha > Kuchapisha Vipengee Mbalimbali > Kuchapisha Karatasi ya Kuandika

Kuchapisha Karatasi ya Kuandika

Unaweza kuchapisha karatasi asili ya kuandika kwa urahisi kkwa picha kutoka kwa kifaa cha kumbukumbu kilichowekwa kama mandharinyuma. Picha hii imechapishwa kihafifu ili kuwa inaweza kuandikwa juu kwa urahisi.

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 2 wa Karatasi

    Kupakia Karatasi katika Nafasi ya Nyuma ya Karatasi

  2. Chomeka kifaa cha kumbukumbu kwenye sloti ya kadi ya SD au kiweko cha USB cha kiolesura cha nje cha kichapishi.

    Kuingiza Kadi ya Kumbukumbu

    Kuchomeka Kifaa cha Nje cha USB

  3. Teua Various Prints kwenye paneli dhibiti.

  4. Teua Personal Stationery > Writing Papers.

  5. Teua aina ya karatasi ya kuandika.

  6. Teua mandharinyuma.

    Chaguo zinatofautiana kwa kutegelea aina ya karatasi ya kuandika.

  7. Fanya moja kati ya yafuatayo kulinagana mandharinyuma uliyochagua katika hatua ya 6.

    Chaguo zinatofautiana kulinagana na aina ya mandharinyuma.

    • Design
      Teua ruwaza, kama vile mipaka au nukta polka au Original Design kisha uteue ruwaza uliyounda kwa kutumia kipengele cha ruwaza ya karatasi.
    • Photo
      Wakati ujumbe unaokuambia kuwa kupakia picha kumekamilika unaonyeshwa, teua OK. Teua , teua picha unayotaka kuchapisha kwenye skrini ya kuteua picha kisha uteue Done. Teua Next.
    • Color
      Teua rangi ya mandharinyuma.
    • No Background
      Nenda kwa hatua inayofuata.
  8. Unda mipangilio ya karatasi.

  9. Ingiza idadi ya nakala, na kisha udonoe .