Soma na ufuate maelekezo haya ili uhakikishe matumizi salama ya kichapishi hiki.Weka mwongozo huu kwa marejeleo ya siku zijazo.Pia, hakikisha unafuata onyo na maagizo yote yaliyowekwa kwenye kichapishi.
Baadhi ya alama zinazotumika kwenye printa yako ni za kuhakikisha usalama na matumizi sahihi ya printa. Tembelea Tovuti ifuatayo ili ujifunze maana ya alama hizi.
Tumia waya ya nishati uliyokuja na printa peke yake na usitumie waya hiyo na kifaa kingine chochote. Utumiaji wa waya zingine kwenye printa hii au utumiaji wa waya ya nishati iliyokuja na kifaa kingine huenda ukasababisha moto au mshtuo wa umeme.
Hakikisha waya yako ya nishati ya AC inatimiza viwango muhimu vya usalama vya eneo.
Usiwahi kufunguanisha, kurekebisha, au kujaribu kukarabati waya ya nishati, plagi, kitengo cha printa, kitengo cha kitambazo, au chaguo wewe mwenyewe, isipokuwa kama ilivyoelezewa hasa katika miongozo ya printa.
Chomoa plagi ya printa na upeleke kwa mtu aliyehitimu kukarabati chini ya hali zifuatazo:
Waya au plagi ya nishati imeharibika; majimaji yameingia katika printa; printa imeangushwa au kesi imeharibika; printa haifanyi kazi kawaifa au inaonyesha tofauti mpya ya utendaji. Usirekebishe udhibiti ambao hauelezwa na maelekezo ya utendaji.
Weka printa karibu na soketi ya ukutani ambapo plagi inaweza kuchomolewa kwa urahisi.
Usiweke au kuhifadhi printa nje, katibu na uchafu au vumbi jingi, majimaji, vyanzo vya moto, au katika maeneo yaliyo na mshtuko, mtetemeko, halijoto ya juu au unyevu.
Chunga usimwagie printa majimaji na usishughulikie printa na mikono yenye majimaji.
Weka printa angalau sentimita 22 mbali na kidhibiti mpigo wa moyo. Mawimbi ya redio kutoka kwa printa hii yanaweza kuathiri ufanyaji kzi wa kidhibiti mpigo wa moya vibaya.
Ikiwa skrini ya LCD imeharibika, wasiliana na muuzaji wako. Ikiwa mchanganyiko angavu wa majimaji utamwagikia mikono yako, ioshe vizuri na sabuni na maji. Ikiwa mchanganyiko angavu wa majimaji utamwagikia mikono yako, yaoshe vizuri na maji mara moja. Ikiwa usumbufu au matatizo ya kuona yataendelea baada ya kuosha macho vizuri, mtembelee daktari mara moja.
Kuwa makini unaposhughulikia katriji zilizotumika za wino, kwani kunaweza kuwa na wino kando ya lango la kutoa wino.
Wino ukikumwagikiwa kwenye ngozi, safisha sehemu hiyo vizuri ukitumia sabuni na maji.
Wino ukiingia ndani ya macho yako, yamwagie maji mara moja. Maumivu au matatizo ya kuona yakiendelea baada ya kuyamwagia maji, mtembelee daktari mara moja.
Wino ukiingia mdomoni mwako, mtembelee daktari mara moja.
Usifungue katriji ya wino na kisanduku cha ukarabati; la sivyo wino unaweza kuingia ndani ya macho yako au kukumwagikia kwenye ngozi.
Usitikise katriji za wino na nguvu na usiziangushe. Pia, chunga usizifinye au kurarua lebo zao. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha uvujaji wa wino.
Weka katriji za wino na kisanduku cha ukarabati mbali na watoto.