> Kuongeza au Kubadilisha Kompyuta au Vifaa > Kuunganisha Kifaa Maizi na Kichapishi Moja kwa Moja (Wi-Fi Direct) > Kuunganisha kwenye Vifaa kando na iOS na Android kwa Kutumia Wi-Fi Direct

Kuunganisha kwenye Vifaa kando na iOS na Android kwa Kutumia Wi-Fi Direct

Mbinu hii hukuruhusu kuunganisha kichapishi moja kwa moja kwenye vifaa maizi bila kipanga njia pasiwaya.

Kumbuka:

Unahitaji kuunda mipangilio hii kwa kichapishi na kifaa maizi unachotaka kuunganisha mara moja. Isipokuwa ulemaze Wi-Fi Direct au kurejesha mipangilio ya mtandao kwa chaguo-msingi yake, huhitaji kuunda mipangilio hii tena.

  1. Donoa Smartphone connect kwenye skrini ya nyumbani.

  2. Donoa Start Setup.

  3. Donoa Other OS Devices.

    SSID na Password kwa Wi-Fi Direct vya kichapishi vinaonyeshwa.

  4. Kwenye skrini ya Wi-Fi ya kifaa maizi, teua SSID iliyoonyeshwa kwenye paneli dhibiti, na kisha uingize nenosiri.

    Picha ya skrini ni mfano kwenye iPhone.

  5. Kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, teua Next.

  6. Kwenye kifaa maizi, washa programu ya uchapishaji ya Epson.

    Mifano ya programu za uchapishaji za Epson

  7. Kwenye skrini ya programu ya uchapishaji ya Epson, donoa Printer is not selected.

  8. Teua kichapishi unachotaka kuunganisha.

    Tazama maelezo yaliyoonyeshwa kwenye paneli dhibiti ya kichapishi ili kuteua kichapishi.

  9. Kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, teua Complete.

Kwa vifaa maizi ambavyo vimeunganishwa kwenye kichapishi mbeleni, teua jina la mtandao (SSID) kwenye skrini ya Wi-Fi ya kifaa maizi ili kuviunganisha tena.