Teua Memory Card Data ili kuonyesha picha kama onyesho slaidi wakati hakuna operesheni zinatekelezwa kwa karibu dakika tatu.
Teua On ili kuwasha kichapishi kiotomatiki kinapopokea kazi ya kuchapisha au kutambaza kupitia kwa muunganisho wa USB au muunganisho wa mtandao. Ili kuanza kuchapisha, unahitaji kutelezesha nje trei towe. Pia, kuwezesha Auto Power On huongeza matumizi ya nishati kiasi kwenye hali ya sinzia ange ikilinganishwa na kuzima kichapishi kabisa.
Tumia mpangilio wa Power Off Timer iwapo unataka kichapishi kuzima kiotomatiki wakati kazi ya kuchapisha au kutambaza imekamilika na kipindi cha muda kilichowekwa kimepita bila operesheni kutekelezwa. Hii ni muhimu wakati uchapishaji kutoka kwa eneo la mali kama vile kupitia mtandao.
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Power Off Settings kulingana na eneo la ununuzi.
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki wakati hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Unaweza kurekebisha muda kabla ya udhibiti wa nishati kutekelezwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Power Off Timer kulingana na eneo la ununuzi.
Power Off If Inactive
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki iwapo hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Power Off If Disconnected
Teua mpangilio huu ili kuzima printa baada ya muda maalum wakati vituo tarishi zote ikijumuisha kituo cha USB kimetenganishwa. Kipengele hiki huenda kisipatiokane kulingana na eneo lako.
Angalia tovuti ifuatayo kwa muda maalum.