Kuchapisha Taswira fifi

Unaweza kuchapisha taswira fifi kama vile (Ya Siri) kwenye uchapishaji wako. Pia unaweza kuongeza taswira fifi yako mwenyewe.

Kumbuka:

Kipengele hiki hakipatikani na uchapishaji usio na mipaka.

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 1 wa Karatasi

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 2 wa Karatasi

    Kupakia Karatasi katika Nafasi ya Nyuma ya Karatasi

  2. Fungua faili unayotaka kuchapisha.

  3. Nenda kwa dirisha la kiendeshi cha kichapishi.

  4. Teua chaguo kutoka kwenye mpangilio wa Chaguo Zaidi.

  5. Bofya Vipengele vya Taswira fifi ili kubadilisha maelezo kama vile uzito na mkao wa taswira fifi.

  6. Weka vipengele hivyo vingine kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi inavyohitajika, na kisha ubofye SAWA.

    Kichupo cha Kuu

    Kichupo cha Chaguo Zaidi

  7. Bofya Chapisha.