> Utambazaji > Kutambaza Nakala Asili kwenye Kifaa Maizi

Kutambaza Nakala Asili kwenye Kifaa Maizi

Unaweza kuhifadhi taswira kuhifadhi taswira zilizotambazwa kwenye kifaa maizi kama vile simu mahiri au kopmyuta kibao.

Kumbuka:
  • Kabla ya kutambaza, sakinisha Epson iPrint kwenye kifaa chako maizi.

  • Skrini za Epson iPrint zinaweza kubadilika bila wewe kuarifiwa.

  • Maudhui ya Epson iPrint yanaweza kuwa tofauti kwa kutegemea bidhaa.

  1. Weka nakala za kwanza.

    Kuweka nakala Asili kwenye glasi ya kichanganuzi

  2. Anzisha Epson iPrint.

  3. Donoa Scan.

  4. Weka mipangilio ya utambazaji. Donoa aikoni ya katika sehemu ya juu kulia ya skrini.

  5. Weka vipengele inavyohitajika.

    • Scanner: Badilisha kitambazaji (kichapishi) unachotaka kutumia.
    • Scanning Size: Teua ukuwa wa nakala asili uliyoweka. Ili kutambaza katika eneo nzima ya glasi ya kitambazaji, teua, MAX.
    • Image type: Chagua rangi unayotaka kutumia kuhifadhi taswira iliyotambazwa.
    • Resolution: Chagua ubainifu.
    • Brightness: Weka ung’avu unapotambaza nakala asili kwenye monokromu.
    • Gamma: Rekebisha miale ya gamma (ung’avu wa safu kati) kwa taswira zilizotambazwa.
  6. Ukimaliza kuweka mipangilio, donoa, Done.

  7. Donoa Scan.

    Kutambaza kunaanza.

  8. Angalia taswira iliyotambazwa, kisha uteue mbinu ya kuhifadhi.

    • : Huonyesha skrini ambapo unaweza kuhifadhi taswira zilizotambazwa.
    • : Huonyesha skrini ambapo unaweza kutuma taswira zilizotambazwa kupitia barua pepe.
    • : Huonyesha skrini ambapo unaweza kuchapisha taswira zilizotambazwa.
  9. Hatimaye, fuata maelekezo kwenye skrini.