Unaweza kuangalia iwapo kiendeshi halali cha kichapishi cha Epson kimesakinishwa kwenye kompyuta yako kwa kutumia mojawapo ya mbinu zifuatazo.
Teua Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi (Vichapishi, Vichapishi na Faksi), na kisha ufuate yafuatayo ili kufungua dirisha la sifa za seva ya kuchapisha.
Windows 10/Windows 8.1/Windows 8/Windows 7
Bofya ikoni ya kichapishi, na kisha ubofye Sifa za seva ya uchapishaji katika upande wa juu wa dirisha.
Windows Vista
Bofya kulia kwenye kabrasha la Vichapishi, na kisha ubofye Endesha kama msimamizi > Sifa za Seva.
Windows XP
Kutoka kwenye menyu ya Faili, teua Sifa za Seva.
Bofya kichupo cha Kiendeshi. Iwapo jina la kichapishi chako litaonyeshwa kwenye orodha, kiendeshi halali cha Epson kimesakinishwa kwenye kompyuta yako.
