Kichupo cha Kuu

Uwekaji Kabla Uchapishaji:

Uwekaji upya wa Kuongeza/Kuondoa:

Unaweza kuongeza au kuondoa uwekaji awali wako kwa mipangilio ya kuchapisha inayotumika kila mara. Teua uwekaji awali unaotaka kutumia kutoka kwenye orodha.

Chanzo cha K'tasi:

Teua chanzo cha karatasi ambacho karatasi huingizwa. Chagua Uteuzi Otomatiki ili kuchagua chanzo cha karatasi kiotomatiki iliyochaguliwa katika mipangilio ya chapisho kwenye kichapishi. Ikiwa umewezesha kitendaji cha Kubadilisha Kaseti Otomatiki kichapishi hulisha karatasi kwenye kichapishi kiotomatiki kutoka kaseti ya karatasi ya 2 wakati karatasi zimeiisha kwenye kaseti ya karatasi ya 1. Pakia karatasi ile ile (aina na ukubwa) katika kaseti ya karatasi ya 1 na kaseti ya karatasi ya 2.

Ukubwa wa Waraka:

Teua ukubwa wa karatasi unayotaka kuchapishwa. Iwapo utateua Mtumiaji-Amefafanuliwa, ingiza upana na urefu wa karatasi.

Isiyo na kingo:

Hukuzwa kiasi kidogo zaidi ya ukubwa wa karatasi ili kusiwe na pambizo zinachapishwa kando ya kingo za karatasi. Bofya Mipangilio ili uteue kiwango cha ukuzaji.

Mwelekeo:

Teua mwelekeo unaotaka kutumia ili kuchapisha.

Aina ya Krtasi:

Teua aina ya karatasi unayochapisha.

Ubora:

Teua ubora wa chapisho unaotaka kutumia kwa uchapishaji. Chaguo zinatofautiana kulinagana na aina ya karatasi.

Kuteua Juu hutoa uchapishaji wa hali ya juu zaidi, lakini kasi ya uchapishaji huenda ikawa ya chini. Iwapo uanataka kuchapisha kwenye karatasi tupu ukitumia ubora wa juu zaidi, teua Bora. Kumbuka kwamba hii inaweza kupungua mno kasi ya kuchapisha.

Rangi:

Teua iwapo utachapisha kwenye rangi au katika monokromu.

Uchapishaji wa Pande 2:

Hukuruhusu kutekeleza uchapishaji wa pande 2.

Settings:

Unaweza kubainisha ukingo wa kuunganisha na pambizo za kuunganisha. Unapochapisha nyaraka za kurasa nyingi, unaweza kuteua kuchapisha kuanzia upande wa mbele au upande wa nyuma wa ukurasa.

Uzito wa Uchapishaji:

Teua aina ya waraka ili kurekebisha uzito wa chapisho. Iwapo uzito wa chapisho unaofaa umeteuliwa, unaweza kuzuia picha kutokea upande wa nyuma. Chagua Mwenyewe ili urekebishe uzito wa chapisho wewe mwenyewe.

Kurasa Nyingi:

Hukuruhusu kuchapisha kurasa nyingi kwenye laha moja au kutekeleza uchapishaji wa bango. Bofya Utaratibu wa Muundo ili kubainisha utaratibu wa kuchapisha kurasa.

Copies:

Weka idadi ya nakala unazotaka kuchapisha.

Pangiliza:

Huchapisha nyaraka nyingi zilizolinganishwa kwa utaratibu na kupangwa kwenye vikundi.

Mpangilio Kinyume:

Hukuruhusu kuchapisha kutoka ukurasa wa mwisho ili kurasa zikusanywe kulingana na mpangilio sahihi baada ya kuchapisha.

Modi Tulivu:

Hupunguza kelele ambayo kicvhapishi hutoa. Hata hivyo, uwezeshaji wa hii unaweza kupunguza kasi ya uchapishaji.

Uhakiki wa Chapisho:

Huonyesha uhakiki wa waraka wako kabla ya kuchapisha.

Laiti ya Kipangaji cha Kazi:

Kipengele cha Job Arranger Lite hukuruhusu kujumuisha faili mbalimbali zilizoundwa na programu tofuti na uzichapishe kama kazi moja ya uchapishaji.

Onyesha Mipangilio/Ficha Mipangilio:

Huonyesha orodha ya vipengee vilivyowekwa sasa kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi. Unaweza kuonyesha au kuficha skrini ya sasa ya orodha ya mipangilio.

Weka upya Chaguo-msingi:

Rejesha mipangilio yote katika thamani chaguomsingi za kiwanda. Mipangilio kwenye kichupo cha Chaguo Zaidi pia hurejeshwa katika chaguomsingi zao.

Viwango vya Wino:

Huonyesha kiwango kinachokadiriwa cha wino.