Kwa kutegemea vipengee, mipangilio ambayo imechaguliwa wakati faili ilikuwa imehifadhiwa kwenye hifadhi bado itatumika kiotomatiki.
Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.
Chaguo za Menyu kwa Tuma/Hifadhi
Hali ya Rangi
Teua iwapo utatambaza kwenye rangi au katika monokromu.
Umbizo la Faili
Teua umbizo la faili.
Mpangilio wa Ukurasa
Unapochagua PDF, Compact PDF, PDF/A, Compact PDF/A, au TIFF kama umbizo la faili, teua iwapo utahifadhi nakala zote asili kama faili moja (kurasa nyingi) au uhifadhi kila nakala asili moja baada ya nyingine (ukurasa mmoja).
Mgao wa Mfinyazo
Teua kiwango cha kubana taswira.
Mipangiliuo ya PDF
Unapoteua PDF kama mpangilio wa kuhifadhi umbizo, tumia mipangilio hii kulinda faili za PDF.
Ili kuunda faili ya PDF ambayo inahitaji nywila wakati wa kufungua, weka Nenosiri la Kufungua Hati. Ili kuunda faili ya PDF ambayo inahitaji nenosiri wakati wa kuchapisha au kuhariri, weka Nenosiri la Vibali.
OCR
Unaweza kuhifadhi picha iliyochanganuliwa kwenye PDF inayoweza kutafutwa. Hii ni PDF ambayo data ya maandishi inayoweza kutafutwa imepachikwa.
Maandishi kwenye nakala asili hutambuliwa kwa kutumia Utambuzi wa Kibambo Chore(OCR), na kisha kupachikwa kwenye taswira iliyochanganuliwa.
Kipengee hiki hakipatikani unapotumia Kwenye Kompyuta, Kwenye Wingu, Kwenye Hifadhi, au menyu ya Kuhamisha kwenye Wingu.
Kumbuka:
Kulingana na nakala asili, huenda maandishi yasitambuliwe ipasavyo.
Lugha: Chagua lugha ya maandishi chanzo ya nakala asili.
Mwelekeo wa Ukurasa: Chagua mwelekeo wa picha ya towe. Teua Uzungushaji Otomatiki kuzungusha picha kiotomatiki ili kulingana na mwelekeo wa maandishi yanayotambuliwa katika nakala asili.