Mipangilio ya Uchapishaji (Windows)

  1. Kwenye kichupo cha kiendeshi cha kichapishi Kuu, teua Settings.

  2. Teua jinsi ya kurekebisha upana wa mpaka kwenye Taswira katika Pambizo ya Kujalidi.

    Badilisha Taswira, Punguza Taswira, Futa Taswira

    Kumbuka:

    Iwapo kuna picha katika nafasi ya kuweka shimo, weka uunganishaji wa mm 18.5 kwa pambizo au zaidi kabla kuchapisha. Unaweza kuweka pambizo ya uunganishaji kuanzia Pambizo ya Kujalidi.

  3. Kwenye kichupo cha Kukamilisha, teua nafasi ya kutoboa shimo kutoka kwenye Toboa.

  4. Weka vipengee vingine, na kisha ubofye SAWA.

  5. Bofya Chapisha.