Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Mipangilio > Matengenezo
Matengenezo
Urekebishaji wa Ubora wa Chapa
Teua kipengele hiki iwapo kuna matatizo yoyote kwa machapisho yako. Unaweza kuangalia nozeli zilizoziba na usafishe kichwa cha kuchapisha ikihitajika, na kisha urekebishe baadhi ya parameta ili kuimarisha ubora.
Ukgz Nozeli ya Kichwa Chapa
Teua kipengele hiki ili iangalie kama nozeli za kichwa cha kuchapisha zimeziba.Kichapishi huchapisha ruwaza ya ukaguzi wa nozeli.
Usafishaji Kichwa cha Chapa
Usafishaji Kichwa
Hurudia otomatiki kukagua nozali na kusafisha kichwa ili kuboresha nozali zilizozibika.
Kumbuka:
Kwa sababu Usafishaji Kichwa unaweza kurudia usafishaji wa kichwa mara nyingi, inaweza kuchukua muda mrefu na kutumia kiwango kikubwa cha wino.
Usafishaji wa Kichwa Kimkono
Teua kipengele hiki ili kusafisha nozeli zilizoziba katika kichwa cha kuchapisha.
Mpangilio uliopigwa Mstari
Teua kipengele hiki ili kupanga mistari ya wima.
Usafishaji wa Mwongozo wa Karatasi
Teua kipengele hiki iwapo kuna madoa ya wino kwenye rola za ndani.Kichapishi huingiza karatasi ili kusafisha rola za ndani.
Ondoa Karatasi
Tumia kipengele hiki ikiwa bado kuna vipande vilivyoraruka vya karatasi ndani ya kichapishi hata baada ya kuondoa karatasi iliyokwama.Kichapishi huongeza nafasi zaidi kati ya kichwa cha kuchapisha na sehemu ya karatasi ili kurahisisha kuondoa vipande vya karatasi vilivyoraruka.
Maelezo ya rola ya kuchukua
Teua kipengee hiki ili kuangalia maisha ya huduma ya rola ya uchukuaji ya kaseti ya karatasi. Unaweza pia kuweka upya kaunta yako ya rola ya uchukuaji.
Urekebishaji wa Ubora wa Chapa kwa kila Karatasi
Kulingana na aina ya karatasi, uzungushaji wa wino hutofautiana. Teua kipengele hiki iwapo kuna bendi kwenye machapisho au kutolingana kwa aina maalum ya karatasi.